title : AKINA MAMA,MBUNGE AZZA WASHIRIKI UJENZI WODI YA WAZAZI NA MTOTO KITUO CHA AFYA TINDE
kiungo : AKINA MAMA,MBUNGE AZZA WASHIRIKI UJENZI WODI YA WAZAZI NA MTOTO KITUO CHA AFYA TINDE
AKINA MAMA,MBUNGE AZZA WASHIRIKI UJENZI WODI YA WAZAZI NA MTOTO KITUO CHA AFYA TINDE
Akina mama zaidi ya 200 wa kijiji cha Jomu kata ya Tinde mkoani Shinyanga wakiongozwa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hamad Hilal (CCM) wameadhimisha wiki ya Wanawake Duniani kwa kushiriki ujenzi wa jengo la wodi ya wazazi na watoto katika kituo cha afya Tinde kwa kujitolea kusomba maji.
Akina mama hao wamejitolea kusomba maji kutoka katika bwawa la Tinde hadi katika kituo hicho cha afya leo Jumatatu Machi 5,2018 siku ambayo mafundi ujenzi wamemwaga jamvi katika jengo hilo la wodi ya wazazi na watoto.
Ujenzi wa jengo hilo unaoendelea ni miongoni mwa majengo yanayojengwa katika kituo hicho ambapo majengo mengine ni jengo la upasuaji,wodi ya wazazi,chumba cha kuhifadhia maiti,maabara na nyumba ya mtumishi ambayo kwa pamoja yatagharimu shilingi milioni 400 zilizotengwa na serikali.
Akizungumza kituoni hapo,Mheshimiwa Azza Hilal Hamad aliwashukuru akina mama hao kujitokeza kusaidia katika ujenzi huo ambao kukamilika kwa jengo hilo kutaondoa adha wanayopata akina mama pindi wanapofika katika kituo hicho kupata huduma za afya.
“Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga tumepata shilingi milioni 900 kwa ajili ya vituo viwili ya afya vya Samuye na Tinde naishukuru sana serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais wetu mpendwa Dkt. John Pombe Magufuli na wasaidizi wake akiwemo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Seleman Jafokwa kuweka kipaumbele huduma ya mama na mtoto”,alieleza.
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa jengo la wodi ya wazazi na watoto katika kituo cha afya Tinde
Wa tano kutoka kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hamad Hilal (CCM) akiwa amebeba ndoo ya maji na akina mama wenzake wakazi wa kijiji cha Jomu wakishiriki ujenzi wa jengo la wazazi na watoto kituo cha afya Tinde
Akina mama wakiwa wamebeba ndoo za maji
Zoezi la kusomba maji likiendelea.
Hivyo makala AKINA MAMA,MBUNGE AZZA WASHIRIKI UJENZI WODI YA WAZAZI NA MTOTO KITUO CHA AFYA TINDE
yaani makala yote AKINA MAMA,MBUNGE AZZA WASHIRIKI UJENZI WODI YA WAZAZI NA MTOTO KITUO CHA AFYA TINDE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala AKINA MAMA,MBUNGE AZZA WASHIRIKI UJENZI WODI YA WAZAZI NA MTOTO KITUO CHA AFYA TINDE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/akina-mamambunge-azza-washiriki-ujenzi.html
0 Response to "AKINA MAMA,MBUNGE AZZA WASHIRIKI UJENZI WODI YA WAZAZI NA MTOTO KITUO CHA AFYA TINDE"
Post a Comment