title : MAMA WA MITINDO APEWA TUZO YA KUTAMBUA MCHANGO WAKE
kiungo : MAMA WA MITINDO APEWA TUZO YA KUTAMBUA MCHANGO WAKE
MAMA WA MITINDO APEWA TUZO YA KUTAMBUA MCHANGO WAKE
Na Ripota Wetu, Globu ya Jamii
ASIA Idarus Khamsin maarufu kwa jina la Mama wa Mitindo amepokea tuzo ya Lifetime achievement award kutoka kwa designers na models wa Tanzania.
Sherehe za kupewa tuzo hiyo zilifanyika Jumapili ya wiki iliyopita kwenye ukumbi wa King Solomon jijini Dar es Salaam ambapo tuzo hiyo pia amepewa kwa kutambua namna alivyokuwa mstari wa mbele kuandaa majukwaaa yanayotoa fursa wanamitindo kutangaza vipaji vyao.
Akizungumza baada ya kupewa tuzo hiyo ya kutambua mchango wake kwenye tasnia ya mitindo, Mama wa Mitindo pamoja na mambo mengine amewashukuru sana wanawe.
Amefafanua amewashukuru kwa sababu ya kumthamini na kuona kwamba alikuwa Mama asiechagua wa kumsaidia."Nitaendelea kuwa pamoja nanyi kwa kuhakikisha nawashauri hasa kuzingatia maadili mema katika mavazi na tasnia nzima,"amesema Mama wa Mitindo.
Wanamitindo na wabunifu wa mavazi waliondaa sherehe na tuzo hiyo wameongozwa na Martin Kadinda,Alabama King, Agusta Masaki, Nelson,Ommystlishy na Rukia Walele ambapo wamesema wamevutiwa na wataendelea kutambua mchango wa Mama Mitindo katika tasnia hiyo.
ASIA Idarus Khamsin maarufu kwa jina la Mama wa Mitindo akiwa katika picha ya pamoha na designers na models wa Tanzania.
ASIA Idarus Khamsin maarufu kwa jina la Mama wa Mitindo aakionesha tuzo ya Lifetime achievement award aliyopewa na designers na models wa Tanzania.
ASIA Idarus Khamsin maarufu kwa jina la Mama wa Mitindo kwa pamoja akifurahia na designers na models wa Tanzania mara baada kukabidhiwa tuzo ya Lifetime achievement award
ASIA Idarus Khamsin maarufu kwa jina la Mama wa Mitindo akimshukuri mmoja wa Waandaji wa hafla hiyo Martin Kadinda
Hivyo makala MAMA WA MITINDO APEWA TUZO YA KUTAMBUA MCHANGO WAKE
yaani makala yote MAMA WA MITINDO APEWA TUZO YA KUTAMBUA MCHANGO WAKE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAMA WA MITINDO APEWA TUZO YA KUTAMBUA MCHANGO WAKE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/mama-wa-mitindo-apewa-tuzo-ya-kutambua.html
0 Response to "MAMA WA MITINDO APEWA TUZO YA KUTAMBUA MCHANGO WAKE"
Post a Comment