Watanzania wahimizwa kujiunga na mtandao wa mitaji

Watanzania wahimizwa kujiunga na mtandao wa mitaji - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Watanzania wahimizwa kujiunga na mtandao wa mitaji, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Watanzania wahimizwa kujiunga na mtandao wa mitaji
kiungo : Watanzania wahimizwa kujiunga na mtandao wa mitaji

soma pia


Watanzania wahimizwa kujiunga na mtandao wa mitaji

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustine Kamuzora amewataka wafanyabiashara nchini kuhamasika kujiunga na mtandao wa mitaji ya ubia ili kuimarisha vitega uchumi vyao na pia kusaidia kuanzisha viwanda hapa nchini.

Profesa Kamuzora alisema hayo wakati akizindua Mtandao wa Mitaji ya Ubia Tanzania – Tanzania Venture Capital Network jijini Dar es salaam jana.Aidha Katibu Mkuu huyo amesema uzinduzi wa mtandao huo umefanyika wakati mwafaka ambapo serikali ya awamu ya tano ipo katika mikakati ya kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya viwanda,

Aliwataka wananchi kuacha uoga katika ushiriki wa kuwawezesha kuwepo kwa mitaji ya kutosha kwa ajili ya uimarishaji wa uwekezaji nchini Tanzania.Alisema serikali kwa sasa inafanya kila linalowezekana kuhakikisha mazingira ya biashara na uwekezaji yanakuwa bora, ndio maana wameanzisha mchakato wa kutengeneza sera ya maendeleo ya viwanda hasa katika sekta binafsi.

Alisema ni vyema wenye viwanda na wananchi wengine kushiriki katika mchakato huo ili kufanikisha nia ya kuipeleka Tanzania katika nchi ya viwanda. Alisema kwa kuwa na sera sheria nyingi zitabadilika na hivyo kupunguza urasimu na pia vikwazo vya kuwezesha kazi katika masuala ya viwanda na biashara.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustine Kamuzora akitoa hotuba ya uzinduzi rasmi wa Mtandao wa Tanzania Venture Capital ambapo amesema umefanyika wakati mwafaka ambapo serikali ya awamu ya tano ipo katika mikakati ya kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya viwanda katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr Reginald Mengi akitoa neno la ufunguzi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustine Kamuzora kutoa hotuba ya uzinduzi wa Mtandao wa Tanzania Venture Capital uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr. Reginald Mengi akibadilisha na mawazo na Afisa Mtendaji Mkuu wa DOB Equity, Brigit van Dijk-van de Reijt wakati wa hafla ya uzinduzi wa wa Mtandao wa Tanzania Venture Capital uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mgeni rasmi Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustine Kamuzora (wa tatu kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya sekta Binafsi nchini-TPSF Bw. Godfrey Simbeye (kushoto).
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini Bw. Godfrey Simbeye (kushoto) akifafanua jambo kabla ya kuanza kwa uzinduzi wa Mtandao wa Mitaji ya Ubia Tanzania – Tanzania Venture Capital Network uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Wanaomsikiliza ni Muasisi wa Mtandao wa Tanzania Venture Capital, Bw. Salum Awadh (wa pili kushoto aliyesimama), Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr Reginald Mengi (wa pili kulia) pamoja Mkurugenzi wa Uwekezaji na Maendeleo ya Viwanda –TPSF, Edward Furaha (kulia).



Hivyo makala Watanzania wahimizwa kujiunga na mtandao wa mitaji

yaani makala yote Watanzania wahimizwa kujiunga na mtandao wa mitaji Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Watanzania wahimizwa kujiunga na mtandao wa mitaji mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/watanzania-wahimizwa-kujiunga-na.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Watanzania wahimizwa kujiunga na mtandao wa mitaji"

Post a Comment