MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA SHIMMUTA

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA SHIMMUTA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA SHIMMUTA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA SHIMMUTA
kiungo : MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA SHIMMUTA

soma pia


MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA SHIMMUTA

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi wa Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi kuwaruhusu wafanyakazi kushiriki michezo katika maeneo yao ya kazi lakini pia wawaruhusu wafanyakazi hao kushiriki Michezo ya SHIMMUTA.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) mjini Dodoma.

Makamu wa Rais amesema michezo ni muhimu sana kwenye Tanzania ya Viwanda kwani michezo husaidia mwili kuwa wenye afya bora na utendaji wao wa kazi unakuwa mzuri zaidi.
Makamu wa Rais amesema yeye alikuwa mwanamichezo mzuri wa mpira wa pete (netball) lakini kwa sasa anafanya mazoezi kidogo kidogo asubuhi na jioni.

“Najua Umuhimu wa kufanya mazoezi kwa sababu nikiacha kufanya mazoezi nadorora na katika nafasi hii ukidorora unadorora mpaka akili na kazi zitakushinda”

Makamu wa Rais aliwasihi Viongozi wa Michezo kusimamia masuala ya michezo katika maeneo ya kazi na kuwataka Viongozi wa Taasisi kuweka bajeti ya michezo kwa ajili ya kushiriki michezo ya SHIMMUTA.

Makamu wa Rais amesema ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya 2015- 2020 imeleekeza kuendeleza michezo sehemu za kazi.

Aidha Mwenyekiti wa SHIMMUTA Ndugu Hamis Mkanachi alimpongeza Makamu wa Rais kwa juhudi anazozifanya katika kukuza michezo nchini.



Hivyo makala MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA SHIMMUTA

yaani makala yote MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA SHIMMUTA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA SHIMMUTA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/makamu-wa-rais-afungua-mkutano-wa_27.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA SHIMMUTA"

Post a Comment