title : KATIBU WA ORGANAZESHENI CCM ZANZIBAR AFANYA ZIARA MKOA WA KASKAZINI UNGUJA.
kiungo : KATIBU WA ORGANAZESHENI CCM ZANZIBAR AFANYA ZIARA MKOA WA KASKAZINI UNGUJA.
KATIBU WA ORGANAZESHENI CCM ZANZIBAR AFANYA ZIARA MKOA WA KASKAZINI UNGUJA.
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Organazesheni CCM Zanzibar ,Ndugu Bakari Hamad Khamis amesema wanachama na watendaji wa CCM wanatakiwa kuandaa mipango endelevu ya kuhakikisha Chama kinashinda na kubaki madarakani katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.
Rai hiyo ameitoa katika ziara yake ya kujitambulisha kwa watendaji wa Chama na Jumuiya zake ambao ni wajumbe wa Sekreterieti za Wilaya na Majimbo ya CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja, amesema Chama Cha Mapinduzi ili kishinde ni lazima maandalizi ya ushindi wake yaanze kwa sasa.
Alieleza kuwa pamoja na mambo mengine lengo la ziara hiyo ni kuwakumbusha watendaji hao majukumu yao ya msingi wanayotakiwa kuyafanyia kazi kabla ya uchaguzi mkuu ujao.
Amesema CCM ikiwa katika mfumo wa vyama vingi vya siasa ni lazima ifanye kazi kwa bidii ili kuleta mabadiliko chanya kwa wananchi wote bila ya ubaguzi.
WATENDAJI wa CCM Wilaya ya Kaskazini ‘A’ wakimkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Katibu wa Kamti Maalum ya NEC, Idara ya organazesheni CCM Zanzibar ndugu Bakari Hamad Khamis katika ziara ya kujitambulisha kwa Secretarieti ya CCM ngazi za majimbo na Wilaya.
BAADHI ya wajumbe wa Sekreterieti za majimbo na Wilaya ya Kaskazini ‘A’ wakimlaki mgeni rasmi mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Wilaya iliyopo Gamba Mkoa wa Kaskazini Unguja.
KATIBU mwenezi CCM Wilaya kASKAZINI ''A'' Ali Chum Haji(kulia aliyesimama akizungumza), Katibu wa idara ya organazesheini CCM Zanzibar Bakar Hamad (katikati).
BAADHI ya wajumbe wa Sekreterieti za majimbo na Wilaya ya Kaskazini ‘A’ wakimlaki wakisikiliza na kufuatilia nasaha za mgeni rasmi.
Katibu wa Kamti Maalum ya NEC, Idara ya organazesheni CCM Zanzibar ndugu Bakari Hamad Khamis akizungumza na watendaji hao katika ziara ya kujitambulisha kwa Secretarieti ya CCM ngazi za majimbo na Wilaya ya Kaskazini ‘’A’’.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala KATIBU WA ORGANAZESHENI CCM ZANZIBAR AFANYA ZIARA MKOA WA KASKAZINI UNGUJA.
yaani makala yote KATIBU WA ORGANAZESHENI CCM ZANZIBAR AFANYA ZIARA MKOA WA KASKAZINI UNGUJA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KATIBU WA ORGANAZESHENI CCM ZANZIBAR AFANYA ZIARA MKOA WA KASKAZINI UNGUJA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/katibu-wa-organazesheni-ccm-zanzibar.html
0 Response to "KATIBU WA ORGANAZESHENI CCM ZANZIBAR AFANYA ZIARA MKOA WA KASKAZINI UNGUJA."
Post a Comment