title : JOHN CHEYO AWAPINGA WANAOTAKA KUANDAMANA APRILI 26
kiungo : JOHN CHEYO AWAPINGA WANAOTAKA KUANDAMANA APRILI 26
JOHN CHEYO AWAPINGA WANAOTAKA KUANDAMANA APRILI 26
Na Emmanuel Masaka,Globu ya Jamii
MWENYEKITI wa Chama cha MAANDAAMANO UDP,John Cheyo amewataka wanaotaka kufanya maandamano Aprili 26 mwaka huu kuacha kwani yatasababisha uvunjifu wa amani nchini.
Cheyo ameamua kuvunja ukimya na hatimaye kukemea wanaotaka kufanya maandamano ambapo amesisitiza na bora wakaacha kufanya.
Kauli ya Cheyo ambayo ameitoa leo inakuja wakati ambao viongozi mbalimbali akiwamo Rais John Magufuli na Mkuu wa Jeshi la Polisi(IGP), Simon Sirro, wakitoa kauli za kuwataka wanaotaka kuandamana siku hiyo kuacha mara moja na iwapo watafanya hivyo watasimulia watakachokipata kwa waliwatuma.
Mwekyekiti huyo, amesema haki haipimwi kwa kuruhusiwa kufanya maandamano au mikutano ya hadhara.“Watanzania tutangulize masilahi ya nchi mbele, amani ndio kila Kitu, tusiruhusu wanaotaka kuvuruga amani, hakuna mahali pazuri pakuishi kama Tanzania."Juzi wenzetu wakenya Rais Uhuru na Odinga walikutana wakasema hakuna zaidi ya Kenya na kukubaliana kudumisha amani.
"Sasa hivi kuna viashiria vya watu kuchoka kuishi kwa amani, vita ya namna hii haifai, nataka utulivu kama huu tulionao watanzania uendelee ili watu waweze kufanya kazi za kujenga Taifa, tuache hofu kwamba hapa hapakaliki,” amsema Cheyo.Aidha amewataka wanaolalamika kwamba sheria zinavunjwa waende mahakamani kulalamika na maandamani si chochote bali uchonganishi.
Pia amewataka viongozi wa dini kuwa wapatanishi kama vitabu vya dini vinavyowatambulisha badala ya kuchochea wananchi wananchi kuvunja sheria kwa kisingizio cha kudai haki.“Kila kitu kinaachofanywa kwa kupitiaa siasa kisiwe kizingizio kwa mambo mengine, viongozi wengine wafanye kama vile ambavyo wamekuwa wakifanya kipindi cha nyuma, wasiwe chanzo cha watu kufarakana,” amesema Cheyo.
Kuhusu viongozi waandamizi wa Serikali kufanya urasimu kwenye baadhi ya mambo na kukwamisha maendeleo alisema viongozi lazima watambue nchi hii inahitaji maendeleo na hivyo hakuna sababu ya kukwamisha mambo.
Hivyo makala JOHN CHEYO AWAPINGA WANAOTAKA KUANDAMANA APRILI 26
yaani makala yote JOHN CHEYO AWAPINGA WANAOTAKA KUANDAMANA APRILI 26 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala JOHN CHEYO AWAPINGA WANAOTAKA KUANDAMANA APRILI 26 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/john-cheyo-awapinga-wanaotaka.html
0 Response to "JOHN CHEYO AWAPINGA WANAOTAKA KUANDAMANA APRILI 26"
Post a Comment