IFAHAMU HALI YA USALAMA NCHI KAMAILIYO TOLEWA NA JESHI LA POLISI

IFAHAMU HALI YA USALAMA NCHI KAMAILIYO TOLEWA NA JESHI LA POLISI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa IFAHAMU HALI YA USALAMA NCHI KAMAILIYO TOLEWA NA JESHI LA POLISI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : IFAHAMU HALI YA USALAMA NCHI KAMAILIYO TOLEWA NA JESHI LA POLISI
kiungo : IFAHAMU HALI YA USALAMA NCHI KAMAILIYO TOLEWA NA JESHI LA POLISI

soma pia


IFAHAMU HALI YA USALAMA NCHI KAMAILIYO TOLEWA NA JESHI LA POLISI



Image result for nsato marijani

Mwambawahabari
Jeshi la polisi limesema kuwa hali ya usalama kwa sasa ni shwari nchini licha ya kuwa na changamoto ndogondogo ambazo kimsingi zimepetiwa suluhisho ambapo takwimu zinaonyesha kuwa katika Kipindi cha januari 2018 makosa makubwa ya jinai yaliyolipotiwa yalikuwa ni 5,238 ikilinganishwa na makosa ya jinai 6,017 yaliyolipotiwa katika Kipindi cha januari 2017.

Akiongea na vyombo vya habari kwa niaba ya Inspekta jenerali wa polisi, kamishina operesheni na mafunzo Nsato Marijani amesema kuwa kutokana na takwimu hizo ni sawa pungufu ya makosa 779 ambayo ni sawa na 12.9% na kuongeza kuwa hiyo inaonyesha juhudi kubwa za serikali zinazofanywa na jeshi la polisi katika kupambana na uhalifu.

Aidha amebainisha kuwa baadhi ya makosa ambayo yalionekana kuwa na idadi kubwa ya matukio kwa Kipindi cha januari mwaka 2017 lakini mwaka huu 2018 yamepungua kwa kiasi kikubwa ni mauaji ambapo yamepungua hadi kufikia matukio 235 kwa Kipindi cha januari kutoka matukio 288 na januari 2017 pungufu ya matukio 53 sawa na 18.4%.

Katika matukio ya ubakaji yamepungua hadi kufikia 588 januari 2018 kutoka matukio 732 januari 2017 pungufu ya matukio 144 sawa na 19.7%, matukio ya uvunjaji yamepungua na kufikia 1315 januari 2018 kutoka matukio 1653 januari 2017 ambayo ni sawa na pungufu ya matukio 338 sawa na 20.4% na matukio ya wizi wa pikipiki yamepungua na kufikia matukio 416 januari 2018 kutoka matukio 467 januari 2017 ambayo ni sawa na pungufu ya matukio 51 sawa na 10.9%.

Pia amefafanua kwamba kuna baadhi ya matukio ambayo yanaongezeka kutokana na juhudi za operasheni zinazofanywa najeshi la polisi ambapo ametaja makosa hayo kuwa ni kupatikana kwa silaha, kupatikana kwa madawa ya kulevya, kupatikana kwa mabomu, uvuvi haramu, magendo, kupatikana na nyara za serikali na wahamiaji haramu ambapo katika Kipindi cha januari makosa hayo yameongezeka na kufikia 1714 ukilinganisha na makosa 1592 januari 2017 ambayo ni sawa na ongezeko la makosa 119 sawa na 7.5%.

Pia kwa upande wa makosa ya usalama barabarani amesema kuwa matukio ya ajali yaliyolipotiwa januari 2018 yalikuwa 404 ukilinganisha na matukio 542 yaliyolipotiwa januari 2017 ambapo ni sawa na upungufu wa matukio 138 sawa na 25.5%, matukio ya ajali zilizosababisha vifo yamepungua na kufikia 138 ukilinganisha na matukio 117 yaliyolipotiwa kwa Kipindi kama hichohicho sawa na pungufu ya matukio 30 sawa na 22.0%, ajali zilizosababisha vifo zilisaidia kupunguza idadi ya watu waliopoteza maisha kwa ajali za barabarani ambapo katika Kipindi cha januari 2018 kumeripotiwa vifo 178 ukilinganisha na idadi ya watu 203 waliopoteza maisha katika Kipindi kama hichohicho 2017 ikiwa ni upungufu wa vifo 25 sawa na 12.3% na kwa upande wa majeruhi idadi ya watu 353 walijeruhiwa ukilinganisha na majeruhi 474 walioripotiwa katika Kipindi kama hichohicho mwaka 2017 sawa na pungufu ya majeruhi 121 sawa na 22.5%.

Aidha ameweka wazi kwamba kupunguza kwa matukio makubwa ya kiharifu kumechangiwa na ushirikiano mzuri waliopata toka kwa raia wema ambao wamekuwa wakitoa taarifa za viashiria vya uharifu, matukio ya kiuharifu, pamoja na taarifa za waharifu ambazo limesaidia kwa kiasi kikubwa kuzuia matukio ya kuhalifu ambayo yalikuwa yatokee.

pia ametoa wito kwa taasisi mbalimbali za serikali, asasi za kiraia, sekta binafsi za ulinzi, vyama vya siasa, madhehebu ya dini na wananchi kwa ujmla kuendelea kutoka ushirikiano na kutoka taarifa zitakazowezesha kukabiliana na uharifu na wahalifu kote nchini.

Aidha amesema kuwa polisi inatoa onyo kwa wale wote wasiopenda kutii sheria kwa hiari yao kuachana na tabia hiyo, wakiwemo madereva wa mabasi ya abiria kwenda mwendo kasi, kujaza kupita uwezo wa kawaida, bodaboda kutokuvaa kofia ngumu kichwani na kupakia abiria zaidi ya mmoja na kukatiza barabarani wakati wa taa nyekundu zimawaka na kusisitiza kuwa wakiendelea na tabia hiyo watashughukikiwa kwa mujibu wa sheria.



Hivyo makala IFAHAMU HALI YA USALAMA NCHI KAMAILIYO TOLEWA NA JESHI LA POLISI

yaani makala yote IFAHAMU HALI YA USALAMA NCHI KAMAILIYO TOLEWA NA JESHI LA POLISI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala IFAHAMU HALI YA USALAMA NCHI KAMAILIYO TOLEWA NA JESHI LA POLISI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/ifahamu-hali-ya-usalama-nchi-kamailiyo.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "IFAHAMU HALI YA USALAMA NCHI KAMAILIYO TOLEWA NA JESHI LA POLISI"

Post a Comment