title : CHUO KIKUU CHA WAISLAMU CHA MOROGORO KUANZISHA KAMPASI KIGAMBONI JIJINI DAR ES SALAAM KATIKA MASOMO YA USIMAMIZI WA BIASHARA.
kiungo : CHUO KIKUU CHA WAISLAMU CHA MOROGORO KUANZISHA KAMPASI KIGAMBONI JIJINI DAR ES SALAAM KATIKA MASOMO YA USIMAMIZI WA BIASHARA.
CHUO KIKUU CHA WAISLAMU CHA MOROGORO KUANZISHA KAMPASI KIGAMBONI JIJINI DAR ES SALAAM KATIKA MASOMO YA USIMAMIZI WA BIASHARA.
Na John Nditi, Morogoro
UONGOZI wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM) kinatarajia kujenga kampasi tawi la Kigamboni, Jijini Dar es Salaam itakayo kutoa shahada mbalimbali za masomo ya usimamizi wa biashara na kwa kuanzia na udahili wa wanafunzi 5,000.
Chuo hicho Kampasi ya Kigamboni ni kuwezesha kupata wataalamu wengi wa usimamizi wa biashara watakaokidhi mahitaji ya soko la ajira katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).
Makamu mkuu wa Chuo Kikuu hicho, Profesa Hamza Njozi,alisema wakati wa uwekeji wa jiwe la msingi kitakapojengwa eneo la Lingato , Kata ya Kisarawe II ,Manispaa ya Kigamboni , Jijini Dar es Salaam.
Profesa Njozi alisema, tangu kuanzishwa kwa Chuo hicho Oktoba 23, 2004 chini ya Mfuko wa Taasisi ya Maendeleo ya Waislamu (MDF) na kilizinduliwa rasmi Oktoba 22, 2005 na Rais wa Serikali ya awamu ya tatu , Benjamin William Mkapa .
Makamu Mkuu wa Chuo hicho alisema, hadi kufikia mahafali ya kumi mwaka jana ,kimeshatoa wahitimu 5,433 wa ngazi ya Shahada, Stashahada na Astashahada ambapo kwa sasa kina zaidi ya wanafunzi 3,000 na uwezo wa chuo ni kuchukua wanafunzi 8,000.
Profesa Njozi alisema , kujengwa kampasi Tawi la Kigamboni kunatarajiwa kuongeza udahili wa wanafunzi wa ndani na n je ya nchi baada ya uongozi wa Chuo kupata eneo la ardhi lenye ukubwa wa ekari 400 kwa ajili ya ujenzi huo.
Makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM) , Profesa Hamza Njozi akipanda mti baada ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Kampasi yake itakayo kutoa shahada mbalimbali za masomo ya usimamizi wa biashara itakayojengwa eneo la Lingato , Kata ya Kisarawe II, Manispaa ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
Makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM) , Profesa Hamza Njozi ( wapili kushoto fulana pundamilia) akibadirishana mawazo na mmoja wa viongozi wa Chuo hicho baada ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa Kampasi ya Kigamboni itakayo kutoa shahada mbalimbali za masomo ya usimamizi wa biashara itakayojengwa eneo la Lingato , Kata ya Kisarawe II ,Manispaa ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wakiume wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM) wakisaidia kubeba tofari hadi eneo la uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Kampasi ya Kigamboni itakayo kutoa shahada mbalimbali za masomo ya usimamizi wa biashara itakayojengwa eneo la Lingato , Kata ya Kisarawe II ,Manispaa ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wanafunzi wakike wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM) wakisaidia kusogeza mfuko wa saruji kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Kampasi yake itakayo kutoa shahada mbalimbali za masomo ya usimamizi wa biashara itakayojengwa eneo la Lingato , Kata ya Kisarawe II ,Manispaa ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala CHUO KIKUU CHA WAISLAMU CHA MOROGORO KUANZISHA KAMPASI KIGAMBONI JIJINI DAR ES SALAAM KATIKA MASOMO YA USIMAMIZI WA BIASHARA.
yaani makala yote CHUO KIKUU CHA WAISLAMU CHA MOROGORO KUANZISHA KAMPASI KIGAMBONI JIJINI DAR ES SALAAM KATIKA MASOMO YA USIMAMIZI WA BIASHARA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala CHUO KIKUU CHA WAISLAMU CHA MOROGORO KUANZISHA KAMPASI KIGAMBONI JIJINI DAR ES SALAAM KATIKA MASOMO YA USIMAMIZI WA BIASHARA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/chuo-kikuu-cha-waislamu-cha-morogoro.html
0 Response to "CHUO KIKUU CHA WAISLAMU CHA MOROGORO KUANZISHA KAMPASI KIGAMBONI JIJINI DAR ES SALAAM KATIKA MASOMO YA USIMAMIZI WA BIASHARA."
Post a Comment