title : BODABODA KUANZA KUTUMIKA KUSAFIRISHA MAKOZI YA TB
kiungo : BODABODA KUANZA KUTUMIKA KUSAFIRISHA MAKOZI YA TB
BODABODA KUANZA KUTUMIKA KUSAFIRISHA MAKOZI YA TB
*Ummy Mwalimu azindua dawa ya TB kwa watoto,aagiza wanafunzi nao kupimwa ugonjwa huo
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema wapo kwenye mchakato wa kuingia mkataba na waendesha bodaboda ili watumike kusafirisha makozi ya Kifua Kikuu(TB) kutoka vituo vya afya kwenda Hospitali kwa ajili ya vipimo.
Pia amezindua rasmi dawa ya TB kwa ajili ya watoto wenye kubainika kuwa na ugojwa huo ambayo ni tamu na ina ladha ya matunda huku akisisitiza umuhimu wa kila mmoja wetu kupambana kutokomeza TB kwani ni janga la kitaifa.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam kwenye mkutano wa watalaam na wadau wa afya na hasa katika ugonjwa wa TB, Waziri Ummy Mwalimu amesema ugonjwa huo ni tishio nchini na duniani kwa ujumla.
Hivyo amesema kuna jitihada mbalimbali ambazo zinafanywa na Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika kukabiliana na ugonjwa huo.
Amesema licha ya kufanikiwa kuwatambua wagonjwa wa TB lakini changamoto kubwa bado wengi wao wanajificha.Hivyo inakuwa ngumu kutambua na ubaya wake TB inaambukizwa kwa hewa.
Amesema takwimu zinaonesha mgonjwa wa TB anaweza kuambukiza watu wengine 20, hivyo kazi inayofanyika sasa ni kuendelea kuelimisha jamii kupima ili kubaini iwapo wana TB au laa.
Pia amesema kutokana na uhaba wa vifaa vya kupima wenye ugonjwa wa TB inalazimu kwenye vitio vya afya baada ya kuchukua makozi ya mtu anayedhaniwa kuwa na ugonjwa huo husafirishwa kwa gari hadi hospitalini.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungungumza wakati wa mkutano wa wadau wa afya waliokuwa wanajadili namna ya kutokomeza Kifua Kikuu(TB) ambapo ametumia mkutano huo kuzindua dawa ya TB kwa watoto waliobainika na watakaobainika kuwa na ugonjwa huo leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akitoa ufafanuzi kabla ya kumpatia dawa ya TB mtoto Salome Makulusi(3) aliyebainika kuwa na ugonjwa huo.Waziri Mwalim amesema dawa ya TB tayari imeingia nchini na leo ameizundua rasmi wa kwanza kushoto ni Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Muhammed Bakari Kambi.
Baadhi ya wadau wa afya hasa wanaojihusisha na tiba ya ugonjwa wa TB wakimsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto leo jijini Dar es Salaam.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala BODABODA KUANZA KUTUMIKA KUSAFIRISHA MAKOZI YA TB
yaani makala yote BODABODA KUANZA KUTUMIKA KUSAFIRISHA MAKOZI YA TB Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BODABODA KUANZA KUTUMIKA KUSAFIRISHA MAKOZI YA TB mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/bodaboda-kuanza-kutumika-kusafirisha.html
0 Response to "BODABODA KUANZA KUTUMIKA KUSAFIRISHA MAKOZI YA TB"
Post a Comment