title : ASANTE ALEX MSAMA TUKUTANE CCM KIRUMBA TAMASHA LA PASAKA APRILI MOJA
kiungo : ASANTE ALEX MSAMA TUKUTANE CCM KIRUMBA TAMASHA LA PASAKA APRILI MOJA
ASANTE ALEX MSAMA TUKUTANE CCM KIRUMBA TAMASHA LA PASAKA APRILI MOJA
Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii
APRILI Moja katika Uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza,macho na masikio ya Watanzania yataelekezwa uwanjani hapo.Kwanini jibu ni moja tu kutakuwa na Tamasha la Pasaka.
Tamasha la Pasaka ambalo limekuwa likiandaliwa na Msama Promotion kila mwaka na kufanyika siku ya Sikuu ya Pasaka.Ni tamasha ambalo limekuwa likiwaweka Watanzania pamoja.
Ni tamasha ambalo msingi wake mkubwa ni kudumisha upendo na mshikamano kwa Watanzania na kila mwaka kumekuwa na kauli mbiu kuhusu tamasha hilo.Kwa kukumbusha tu kauli mbiu kwenye tamasha la Pasaka kwa mwaka jana ilikuwa inasema hivi "Umoja na upendo kudumisha amani ndani ya nchi yetu" ...na lilifanyika jijini Dar es Salaam, Mwanza na mikoa mingine kwa siku tofauti .
Tamasha la Pasaka la mwaka huu ambalo sasa linafanyika Mwanza kwa mara ya kwanza kauli mbiu yake inasema “UMOJA NA UPENDO HUDUMISHA AMANI KATIKA NCHI YETU” na sababu kubwa ni kwamba Msama Promotion inataka kuwahubiria injili ya Amani na Upendo wakazi wa Kanda ya Ziwana na Vitongoji vyake.
Ukweli ni kwamba msingi mkuu wa Tamasha la Pasaka ni kutumia tamasha hilo kwa ajili ya kuabudu na kumtukuza Mungu.Hivyo ni tamasha ambalo linahusisha zaidi waimbaji wa nyimbo za Injili huku waalikwa mbalimbali wakiwemo viongozi Maaskofu na wachungaji wakitoa jumbe nyingi za kuhumiza Upendo, Amani na Utulivu kwa watanzania.
Kampuni ya Msama Promotioni kupitia Mkurugenzi wake Alex Msama imekuwa ikifanya jitihada za kuhakikisha wanaohudhuria tamasha hilo wanaburudika kutokana na aina ya waimbaji ambao hupata nafasi ya kutumbuiza kwa kuimba nyimbo za Injili katika tamasha hilo.
Waimbaji wengi maarufu wa muziki huo kutoka ndani na nje ya Tanzania wamekuwa wakishiriki kila mwaka kwenye Tamasha la Pasaka.Tamasha ambalo mwaka huu ni la 18 tangu kuanzishwa kwake
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumzia maandalizi ya Tamasha la Pasaka litakalofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba Aprili 1 Jijini Mwanza na Aprili 2 Uwanja wa Halmashauri mjini Bariadi mkoani Simiyu huku akiwatangaza baadhi ya waimbaji katika tamasha hilo kushoto ni mwimbaji Beatrice Mwaipaja na kulia ni Mwimbaji Paul Clement.
Beatrice Mwaipaja kushoto na Mwimbaji Paul Clement. wakizungumza na waandishiwa habari kuhusu maandalizia ya Tamasha la Pasaka.
Hivyo makala ASANTE ALEX MSAMA TUKUTANE CCM KIRUMBA TAMASHA LA PASAKA APRILI MOJA
yaani makala yote ASANTE ALEX MSAMA TUKUTANE CCM KIRUMBA TAMASHA LA PASAKA APRILI MOJA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ASANTE ALEX MSAMA TUKUTANE CCM KIRUMBA TAMASHA LA PASAKA APRILI MOJA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/asante-alex-msama-tukutane-ccm-kirumba.html
0 Response to "ASANTE ALEX MSAMA TUKUTANE CCM KIRUMBA TAMASHA LA PASAKA APRILI MOJA"
Post a Comment