title : WAZIRI MKUU USO KWA USO NA WADAU WA PAMBA JIJIN MWANZA
kiungo : WAZIRI MKUU USO KWA USO NA WADAU WA PAMBA JIJIN MWANZA
WAZIRI MKUU USO KWA USO NA WADAU WA PAMBA JIJIN MWANZA
WAZIRI Mkuu Kassimu Majaliwa, ameitisha kikao cha wadau wa pamba nchini, ili kujadili namna bora ya kuongeza tija ya zao hilo.
Kikao hicho kitakachofanyika jijini Mwanza Februari 15 hadi 16, 2018, kinatarajiwa kuondoa sintofahamu iliyogubika sekta ya pamba, kuhusu mustakabari wa kilimo cha mkataba kutokana na kusudio la Serikali kuanzisha ununuzi wa pamba kwa njia ya mnada kupitia vyama vya ushirika.
Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya kuonesha kusudio la kusitisha kilimo cha mkataba, na uwezekano wa pamba kuuzwa kwa njia ya mnada.Kulingana na taarifa iliyotolewa jana na Waziri wa Kilimo, Dk. Charles Tizeba, kikao hicho muhimu kimelenga kuondoa hali ya sintofahamu, juu ya kilimo cha mkataba na uuzwaji wa zao hilo kwa njia ya mnada.
Kusudio hilo la Serikali la kuuzwa pamba kwa njia yamnada, limeonekana kuleta wasiwasi kwa makampuni yaliyowekeza kwenye sekta hiyo muhimu katika uchumi wa nchi.
Mkoa wa Tabora Agrey Mwanri akifafanua jambo kwa Waziri wa Kilimo Charles Tizeba kabla ya kuanza ziara ya kuona utekelezaji wa kilimo cha Pamba na uzalishaji wa mbegu bora za pamba za UKM08 Msimu 2017/2018 uliofanyika jana tarehe 04 feb 2018.
Akiwa ameambatana na mwenyeji wake Mkuu wa mkoa huo Agrey Mwanri, Waziri Tizeba pia alipata nafasi ya kuzungumza na baadhi ya wakulima na kugundua kuwa bado elimu ya unyunyiziaji dawa haijakaa sawa.
"Tunakwenda kujadiliana nao wanunuzi hawa wa pamba, hususani walioingia kilimo cha mkataba. Asilimia 40 ya Watanzania wote wanategemea uchumi wao kupitia pamba," alisema Waziri Tizeba.Alikuwa akizungumza muda mfupi baada ya kuwasili kwa ziara ya kukagua mafanikio ya zao la pamba, Wilaya ya Igunga mkoani Tabora.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Gaki Investment inayojihusisha na ununuzi wa pamba, Gasper Gaki, alisema: “Tunakingoja kwa hamu sana kikao hiki na Waziri Mkuu, naamini kitakuwa na mafanikio.”Katika hatua nyingine, Waziri huyo mwenye dhamana ya Kilimo alisifu juhudi za kilimo cha pamba, ambapo Mkoa wa Tabora umevuka lengo lake la uzalishaji zao hilo.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WAZIRI MKUU USO KWA USO NA WADAU WA PAMBA JIJIN MWANZA
yaani makala yote WAZIRI MKUU USO KWA USO NA WADAU WA PAMBA JIJIN MWANZA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU USO KWA USO NA WADAU WA PAMBA JIJIN MWANZA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/waziri-mkuu-uso-kwa-uso-na-wadau-wa.html
0 Response to "WAZIRI MKUU USO KWA USO NA WADAU WA PAMBA JIJIN MWANZA"
Post a Comment