title : WAZIRI MKUU AZINDUA MPANGO MKAKATI AFYA MOJA
kiungo : WAZIRI MKUU AZINDUA MPANGO MKAKATI AFYA MOJA
WAZIRI MKUU AZINDUA MPANGO MKAKATI AFYA MOJA
Na Said Mwishehe, Blogu ya jamii
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha Tanzania inakuwa mahala salama na penye afya bora huku akielezea jitihada zinazochukuliwa kukabiliana na magonjwa ya mlipuko na matukio hatarishi kwa wananchi.
Ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam, wakati anazindua Mpango Mkakati wa Afya Moja na Dawati la Kuratibu Afya Moja nchini huku akisisitiza uzinduzi huo ni muhimu hasa kupindi hiki ambacho kumekuwepo na muingiliano mkubwa kati ya binadamu, wanyama na mazingira.
Amesema dhana ya dhana ya Afya Moja inafaa kutumika zaidi katika nchi zinazoendelea kwani inatoa fursa kwa wadau mbalimbali kushirikana katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko.
"Mpango huu wa Afya Moja ni ajenda ambayo ipo kwenye nchi mbalimbali duniani na kwa Tanzania ni mpango ambao tunaamini utasaidia kukabiliana na magonjwa ya mlipuko yatokanayo na binadamu, wanyama na mazingira,"amesema Waziri Mkuu Majaliwa.
Ameongeza mkakati wa kukabiliana na maradhi yatokanayo na wanyama na mazingira ni muhimu kwa nchi nyingi za Afrika kwani zipo kwenye hatari zaidi.
Amesema katika Bara la Afrika kuna maeneo mengi yenye mapori makubwa ,hivyo ni rahisi kuwepo kwa magonjwa ya kuambukizwa yanayotokana na binadamu, wanyama na mazingira,hivyo Afya Moja imekuja wakati sahihi.
Ametoa mfano wa mapori makubwa yaliyopo kwenye Bonde la Mto Kongo, ambalo mazingira yake yamekuwa ni kitovu cha magonjwa ya mlipuko kama vile Ebola, Homa ya Bonde la Ufa (RVF), Marburg na mengineyo.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WAZIRI MKUU AZINDUA MPANGO MKAKATI AFYA MOJA
yaani makala yote WAZIRI MKUU AZINDUA MPANGO MKAKATI AFYA MOJA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU AZINDUA MPANGO MKAKATI AFYA MOJA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/waziri-mkuu-azindua-mpango-mkakati-afya.html
0 Response to "WAZIRI MKUU AZINDUA MPANGO MKAKATI AFYA MOJA"
Post a Comment