title : MVUA, UPEPO WALETA TAFRANI NAMTUMBO
kiungo : MVUA, UPEPO WALETA TAFRANI NAMTUMBO
MVUA, UPEPO WALETA TAFRANI NAMTUMBO
NA YEREMIAS NGERANGERA
Upepo mkali ulioambatana na mvua umeleta tafrani katika kijiji cha Njalamatata kata ya Mkongo Nakawale wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma .
Tafrani hiyo ilitokea siku ya jumatatu wiki hii baada ya nyumba tano kuezuliwa na upepo na wananchi waliokumbwa na dhahama hiyo kubaki wakitafuta makadhi ya kujihifadhi kwa majirani.
Katibu tawala wa wilaya ya Namtumbo bwana Adelin Nchimbi akiwa na kamati ya ulinzi na usalama walifika eneo la tukio na kuongea na waathirika wa tukio la kuezuliwa nyumba katika kijiji cha Njalamatata.
Aidha bwana Nchimbi alisema kuwa katika tukio hilo Nyumba tano ziliezuliwa na upepo lakini hapakujitokeza mwananchi yoyote kujeruhiwa au kuwepo kwa maafa katika tukio hilo.
Alitaja majina ya wananchi walioathirika katika tukio hilo ni Clavery Ponera ,Donatus Kapinga,James Mdagi ,Sadiki Kapinga ,Rusti Kimbili na Lotary Hongo wote ni wakazi wa kijiji hicho cha Njalamatata wilayani humo.
Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Namtumbo pamoja na kutoa pole kwa waathirika wa tukio hilo ilifanya mahojiano na waathirika kubaini hasara iliyopatikana kutokana na tukio hilo.
Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Namtumbo pamoja na pole hizo iliwashauri wananchi wa kijiji hicho kujenga nyumba na kuziezeka kwa kuweka tengo za kushikizia kwenye ukuta baada ya kubaini baadhi ya nyumba hazikuwekwa tengo hizo.
Hivyo makala MVUA, UPEPO WALETA TAFRANI NAMTUMBO
yaani makala yote MVUA, UPEPO WALETA TAFRANI NAMTUMBO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MVUA, UPEPO WALETA TAFRANI NAMTUMBO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/mvua-upepo-waleta-tafrani-namtumbo.html
0 Response to "MVUA, UPEPO WALETA TAFRANI NAMTUMBO"
Post a Comment