title : WANAWAKE GAIRO WAONGOZA KIMKOA KUJIFUNGUA WAKIWA NA UMRI CHINI YA MIAKA 20
kiungo : WANAWAKE GAIRO WAONGOZA KIMKOA KUJIFUNGUA WAKIWA NA UMRI CHINI YA MIAKA 20
WANAWAKE GAIRO WAONGOZA KIMKOA KUJIFUNGUA WAKIWA NA UMRI CHINI YA MIAKA 20
Na John Nditi, Gairo
WANAWAKE wajawazito 2,600 sawa na asilimia 27 kati ya 9,577 waliojifungulia zahanati na vituo vya afya kwa mwaka 2017 katika halmashauri ya wilaya ya Gairo , mkoani Morogoro walibainika kuwa chini umri wa miaka 20.
Hali hiyo ilisababisha kujitokeza kwa vifo vitokanavyo na uzazi pingamizi unaochagiwa na uchungu mkali, kutokwa damu nyingi baada ya kujifungua na kifafa cha mimba.
Mratibu wa Afya ya Mama na Mtoto wa wilaya ya Gairo, Edifonzia Mhafigwa alisema hayo wakati akiwasilisha taarifa katika mkutano wa kujadili utoaji wa elimu kuhusu kutokomeza vifo vitokanavyo na uzazi kwenye siku ya Utepe Mweupe ambayo kimkoa ilifanyika katika kata ya Ukwamani , wilayani humo.
Mbali na changamoto hiyo, wanawake wajawazito waliojifungulia kwa wakunga wa jadi kwa mwaka 2017 walifikia 1,270 , waliojifungulia njiani ni 108 , waliojifungulia nyumbani ni 180 na kwenye Zahanati walikuwa ni 3,482.
Katibu Tawala wa wilaya ya Gairo, mkoani Morogoro, Adam Bibangamba ( aliyesimama) akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa mjadala wa elimu juu ya njia ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi pingamizi kwa wanawake wajawazito na kupinga mimba za utotoni wakati wa siku ya utepe mweupe iliyofanyika kata ya Ukwamani , wilayani humo. ( Picha na John Nditi).
Mkazi wa Kata ya Ukwamani , wilaya ya Gairo akichangia mada
Baadhi ya wananchi wa kata ya Ukwamani , wilaya ya Gairo, mkoani Morogoro wakisiiliza na kusoma vipeperushi vya elimu ya njia ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi vya akina mama wajawazito na kupinga mimba za utotoni, wakati wa mjadala wa uelimisghaji jamiii siku ya utepe mweupe iliyofanyika kwenye kata hiyo.
Wazee wa kata ya Ukwamani, wilaya ya Gairo, mkoani Morogoro ( mstari wa mbele ) wakiwasikiliza wataalamu wa afya ( hawapo pichani) wakati wa utoaji wa elimu ya njia ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi pingamizi kwa akina mama wajawazito na kupinga vita kujifungulia kwa wakunga wa jadi na mimba za utotoni, wakati wa siku ya utepe mweupe iliyofanyika kwenye kata hiyo.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WANAWAKE GAIRO WAONGOZA KIMKOA KUJIFUNGUA WAKIWA NA UMRI CHINI YA MIAKA 20
yaani makala yote WANAWAKE GAIRO WAONGOZA KIMKOA KUJIFUNGUA WAKIWA NA UMRI CHINI YA MIAKA 20 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANAWAKE GAIRO WAONGOZA KIMKOA KUJIFUNGUA WAKIWA NA UMRI CHINI YA MIAKA 20 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/wanawake-gairo-waongoza-kimkoa.html
0 Response to "WANAWAKE GAIRO WAONGOZA KIMKOA KUJIFUNGUA WAKIWA NA UMRI CHINI YA MIAKA 20"
Post a Comment