UZALISHAJI WA PAMBA KUONGEZEKA MARA TANO

UZALISHAJI WA PAMBA KUONGEZEKA MARA TANO - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa UZALISHAJI WA PAMBA KUONGEZEKA MARA TANO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : UZALISHAJI WA PAMBA KUONGEZEKA MARA TANO
kiungo : UZALISHAJI WA PAMBA KUONGEZEKA MARA TANO

soma pia


UZALISHAJI WA PAMBA KUONGEZEKA MARA TANO

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akipulizia dawa shamba la pamba wilayani Kwimba. Uzalishaji wa pamba nchini unatarajiwa kuongezeka mara tano msimu huu wa kilimo 2017/2018 kutokana na juhudi mbalimbali zilizofanywa na Bodi ya Pamba kuhamasisha wakulima kuachana na kilimo cha mazoea na kuanza kuzingatia kanuni za kilimo bora cha pamba, kuimarika kwa mfumo wa upatikanaji na usambazaji wa pembejeo, ubora wa mbegu za kupanda zilizosambazwa kwa wakulima na kuongezeka kwa eneo la uzalishaji wa pamba. 

Akiongea katika ziara ya kukagua maendeleo ya uzalishaji wa mbegu bora wilayani Igunga, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Tanzania Bwana Marco Mtunga amesema, uzalishaji unatarajiwa kuongezeka kwa takriban asilimia 400 kutoka tani 133,000 zilizozalishwa msimu wa 2016/17 hadi kufikia zaidi ya tani 600,000 msimu huu wa 2017/18.

 Aliendelea kueleza kwamba, eneo la uzalishaji wa pamba limeongezeka kutoka ekari 659,000 hadi ekari 3,000,000 ambapo jumla ya tani 26,500 za mbegu zimepandwa zikiwemo tani 8,000 za mbegu za msimu uliopita zilizokuwa kwa wakulima. Kuongezeka kwa eneo la uzalishaji wa pamba kumetokana na uhamasishaji uliofanywa katika maeneo inakolimwa pamba, kuongezeka kwa mikoa mipya ya Dodoma na Katavi katika uzalishaji wa pamba na bei nzuri ya pamba waliyolipwa wakulima msimu uliopita.
Waziri wa Kilimo, Eng. Charles Tizeba, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba, Marco Mtunga na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri wakiongea na mkulima wa pamba wilayani Igunga. 
Waziri wa Kilimo, Eng. Charles Tizeba na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba, Marco Mtunga wakikagua zao la pamba wilayani Igunga. 
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella na Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Mtemi Msafiri wakikagua shamba la pamba wilayani Kwimba 




Hivyo makala UZALISHAJI WA PAMBA KUONGEZEKA MARA TANO

yaani makala yote UZALISHAJI WA PAMBA KUONGEZEKA MARA TANO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala UZALISHAJI WA PAMBA KUONGEZEKA MARA TANO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/uzalishaji-wa-pamba-kuongezeka-mara-tano.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "UZALISHAJI WA PAMBA KUONGEZEKA MARA TANO"

Post a Comment