MRADI ORIO MUARUBAINI TATIZO LA UMEME MKOANI KATAVI

MRADI ORIO MUARUBAINI TATIZO LA UMEME MKOANI KATAVI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MRADI ORIO MUARUBAINI TATIZO LA UMEME MKOANI KATAVI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MRADI ORIO MUARUBAINI TATIZO LA UMEME MKOANI KATAVI
kiungo : MRADI ORIO MUARUBAINI TATIZO LA UMEME MKOANI KATAVI

soma pia


MRADI ORIO MUARUBAINI TATIZO LA UMEME MKOANI KATAVI

 NA SAMIA CHANDE, KATAVI.

Mradi wa Orio uliotekelezwa kwa ushirikiano wa  Serikali ya Uholanzi na Tanzania  kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) umesaidia kujenga kituo cha kuzalisha umeme chenye uwezo wa Megawati 2.5 ambazo zimesaidia  kumaliza tatizo la umeme Wilaya ya  Mpanda na Mkoa wa Katavi kwa ujumla.


Kwa mujibu wa Meneja wa TANESCO Mkoani  Katavi, Mhandisi Julius Sabu, kituo hicho kimesaidia kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme Mkoani humo, na kutoa umeme wa uhakika na wenye ubora.“Kituo hicho kinahudumia Wilaya za Tanganyika, Mpanda mjini, maeneo ya Starlike na Kakese”. Aliainisha Mhandisi Sabu.

Lakini pia Kituo kimepunguza gharama za uzalishaji umeme ukilinganisha na Kituo cha zamani.Wakaazi wa Wilaya ya Tanganyika wameishukuru Serikali na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) kwa kuwaletea umeme kwani umekuwa mkombozi katika shughuli zao za kiuchumi, kama vile kuchomelea, "saloon",  na biashara ya maduka.

“Nawashauri Wananchi wenzangu, sasa ni wakati wa kuchangamkia fursa hii inayotokana na kupata umeme wa uhakika katika kukuza shughuli zetu za kiuchumi.” Alisema Mwananchi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Maneno Mtogwa mkazi wa Wilaya ya Tanganyika.

Meneja wa TANESCO Mkoa wa Katavi ametoa rai kwa Wananchi wa Wilaya za Tanganyika, Mpanda Mjini, maeneo ya Kakese na Starlike kujitokeza kwa wingi kwenye madawati ya huduma kwa Wateja na Ofisi za TANESCO ili kupatiwa huduma kwani TANESCO imejipanga kuwahudumia Wananchi popote walipo na kwa viwango vya hali ya juu.
 Meneja wa TANESCO Mkoa wa Katavi Mhandisi Julius Sabu kiwa anakagua mashine kwenye kituo cha kuzalisha umeme cha Mpanda mkoani Katavi.

 Kituo cha kufua umeme cha Mpanda Mkoani Katavi

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala MRADI ORIO MUARUBAINI TATIZO LA UMEME MKOANI KATAVI

yaani makala yote MRADI ORIO MUARUBAINI TATIZO LA UMEME MKOANI KATAVI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MRADI ORIO MUARUBAINI TATIZO LA UMEME MKOANI KATAVI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/mradi-orio-muarubaini-tatizo-la-umeme.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MRADI ORIO MUARUBAINI TATIZO LA UMEME MKOANI KATAVI"

Post a Comment