title : SHONZA: Umiliki wa Viwanja vya Michezo nchini umezingatia Sheria
kiungo : SHONZA: Umiliki wa Viwanja vya Michezo nchini umezingatia Sheria
SHONZA: Umiliki wa Viwanja vya Michezo nchini umezingatia Sheria
Na Lorietha Laurence-Dodoma
Serikali imeeleza kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kama zilivyo taasisi nyingine kimefuata taratibu za ujenzi na umiliki wa viwanja vya michezo kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni zilizopo.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe .Juliana Shonza leo Mkoani Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Lupa Victor Mwambalaswa, lililohoji kuhusu viwanja vya michezo vinavyomilikiwa na Chama hicho.
“Ni vizuri ikafahamika kwamba mpaka sasa viwanja hivyo vinaendelea kutumika na umma wa watanzania kwa shughuli mbalimbali za kimichezo, kijamii na kiserikali sawa kabisa na Mipango ya Sera ya Maendeleo ya Michezo ya Mwaka 1995, Sura ya 4 (i)-(ii)”
“kwa hiyo kuhusu suala la uporaji wa viwanja hivyo, CCM hakijafanya uporaji wowote kwa kuwa kinamiliki viwanja hivyo kihalali kwa mujibu wa sheria zilizopo hivyo ushiriki wa wananchi wenye mapenzi mema katika ujenzi wa viwanja hivyo hauondoi uhalali wa Chama cha Mapinduzi kumiliki viwanja hivyo”amefafanua Shonza.
Hivyo makala SHONZA: Umiliki wa Viwanja vya Michezo nchini umezingatia Sheria
yaani makala yote SHONZA: Umiliki wa Viwanja vya Michezo nchini umezingatia Sheria Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SHONZA: Umiliki wa Viwanja vya Michezo nchini umezingatia Sheria mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/shonza-umiliki-wa-viwanja-vya-michezo.html
0 Response to "SHONZA: Umiliki wa Viwanja vya Michezo nchini umezingatia Sheria"
Post a Comment