title : SHAHIDI ADAI WEMA ANATUMIA BANGI KAMA STAREHE
kiungo : SHAHIDI ADAI WEMA ANATUMIA BANGI KAMA STAREHE
SHAHIDI ADAI WEMA ANATUMIA BANGI KAMA STAREHE
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa, msanii wa Filamu na Miss Tanzania mwaka 2006 Wema Sepetu alimueleza askari polisi kuwa anatumia bangi kama starehe.
Shahidi wa tatu wa upande wa mashtaka, WP 6441 DC Mary (35) ameyaeleza hayo leo Februari 26 mwaka huu alipokuwa akitoa ushahidi wake katika kesi ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili Wema na wafanyakazi wake wawili.
Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, WP Mary amedai, Februari 4, 2017 alipewa maelekezo na mkuu wake wa kazi OC CID Denis Mujumba kumtoa Wema mahabusu na kwenda nyumbani kwake kufanya upekezi.
Amedai waliondoka yeye, OC CID Mujumba, Inspekta Wille, Koplo Robert na DC Hassan na kuwa wkiwaa njiani alimuuliza Wema kuhusu tuhuma zinazo mkabili kama anahusika na uuzaji wa dawa za kulevya ama kutumia.
Shahidi huyo alieleza, Wema alimjibu kuwa yeye hajishughulishi na uuzaji wa dawa za kulevya ila anatumia bangi kama starehe.Alidai kuwa alimuuliza Wema kuwa ni lini ilikuwa mara mwisho kutumia bangi nakwamba siku hiyo ilikuwa Jumamosi ya Februari 4,mwaka 2017 na Wema alimwambia kuwa Mara ya mwisho kutumia bangi ilikuwa siku ya Jumatatu.
Hivyo makala SHAHIDI ADAI WEMA ANATUMIA BANGI KAMA STAREHE
yaani makala yote SHAHIDI ADAI WEMA ANATUMIA BANGI KAMA STAREHE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SHAHIDI ADAI WEMA ANATUMIA BANGI KAMA STAREHE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/shahidi-adai-wema-anatumia-bangi-kama.html
0 Response to "SHAHIDI ADAI WEMA ANATUMIA BANGI KAMA STAREHE"
Post a Comment