SERIKALI YAADHIMIA KUKUSANYA TAKWIMU ZA AFYA KIELEKTRONIKI NCHI NZIMA.

SERIKALI YAADHIMIA KUKUSANYA TAKWIMU ZA AFYA KIELEKTRONIKI NCHI NZIMA. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI YAADHIMIA KUKUSANYA TAKWIMU ZA AFYA KIELEKTRONIKI NCHI NZIMA., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI YAADHIMIA KUKUSANYA TAKWIMU ZA AFYA KIELEKTRONIKI NCHI NZIMA.
kiungo : SERIKALI YAADHIMIA KUKUSANYA TAKWIMU ZA AFYA KIELEKTRONIKI NCHI NZIMA.

soma pia


SERIKALI YAADHIMIA KUKUSANYA TAKWIMU ZA AFYA KIELEKTRONIKI NCHI NZIMA.



Mwambawahabari 
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imeadhimia kukusanya na kutumia takwimu  kwa njia ya kielektroniki nchi nzima ili kuweza kumudu na kutoa huduma za afya kwa ubora zaidi nchini.


Hayo yamezungumzwa na Katibu Mkuu Wizara ya afya Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati wa kutia Sahihi ya makubaliano ya kuanzisha mfumo wa ukusanyaji takwimu za afya utakaotekelezwa na Wizara ya afya,Wadau wa Maendeleo,Asasi za Kiraia na Shirika la Afya Duniani (WHO) ambao umefanyika leo jijini Dar es salaam.

“Takwimu ni muhimu sana ambazo zitazomuwezesha mtoa huduma kujua mgonjwa historia yake ya ugonjwa  na matibabu aliyopewa awali,kuwapa Uwezo utumishi kujua tunahitaji rasilimali watu kwa kiasi gani  katika kituo cha Afya” alisema Dkt. Ulisubsya.

Aidha, Dkt. Ulisubisya amesema kuwa zoezi hilo litaanza kwenye mikoa ya Tanga,Kilimanjaro na Manyara hatimaye kufikia nchi nzima mpaka kufika 2020 ili kuweza kuwa  na takwimu za afya.

Dkt. Ulisubisya amesema kuwa mfumo wa kujaza takwimu kwenye makaratasi umepitwa na wakati kwani kadri makaratasi ya takwimu yanavyokuwa mengi na makosa ya utoaji huduma yanaweza kutokea  kwani mpaka uanze kutafuta takwimu zilizopita inachukua muda mrefu tofauti na kuhifadhi takwimu kielektroniki.

Mbali na hayo Dkt. Ulisubisya amesema kuwa mpaka hivi sasa hali ya utoaji wa chanjo imefikia asilimia 97 na lengo letu ni kufikia asilimia 100 kupitia mfumo huu wa kukusanya takwimu kwa njia ya kielektroniki.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Matthieu Kamwa amesema kuwa wapo  tayari kushirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya katika kutekeleza hilo ili kuweza kuboresha mifumo ya afya nchini.

“Unajua Takwimu ni utajiri hasa katika kutekeleza shughuli za kutoa huduma za afya kwa wananchi hivyo hatuna budi kuunga mkono juhudu za Serikali ya Tanzania katika kufanikisha jambo hili kwani litaturahisishia hata sisi katika kutoa miongozo ya afya” alisema Dkt. Kamwa.


Hivyo makala SERIKALI YAADHIMIA KUKUSANYA TAKWIMU ZA AFYA KIELEKTRONIKI NCHI NZIMA.

yaani makala yote SERIKALI YAADHIMIA KUKUSANYA TAKWIMU ZA AFYA KIELEKTRONIKI NCHI NZIMA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YAADHIMIA KUKUSANYA TAKWIMU ZA AFYA KIELEKTRONIKI NCHI NZIMA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/serikali-yaadhimia-kukusanya-takwimu-za.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SERIKALI YAADHIMIA KUKUSANYA TAKWIMU ZA AFYA KIELEKTRONIKI NCHI NZIMA."

Post a Comment