Mtandao wa Wanawake na Katiba wajadiliana na wahariri Dar

Mtandao wa Wanawake na Katiba wajadiliana na wahariri Dar - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mtandao wa Wanawake na Katiba wajadiliana na wahariri Dar, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mtandao wa Wanawake na Katiba wajadiliana na wahariri Dar
kiungo : Mtandao wa Wanawake na Katiba wajadiliana na wahariri Dar

soma pia


Mtandao wa Wanawake na Katiba wajadiliana na wahariri Dar

 MTANDAO wa wanawake na katiba/uchaguzi na uongozi leo umekutana na wahariri wa habari na waandishi waandamizi kujadiliana masuala mbalimbali juu ya umuhimu wa kuzingatia misingi na usawa wa kijinsia katika siasa na uongozi nchini.

Akiwasilisha mada kwa wahariri na wanahabari waandamizi katika mkutano huo, mtoa mada na mjumbe wa WFT, Dk. Dinah Richard Mmbaga aliwataka wanahabari kuangalia mfumo mzima wa siasa za vyama vingi na nini kinachoitenganisha siasa ya Tanzania na nchi nyingine bila kujali tofauti za itikadi za vyama kwenye masuala yanayohusu utu wa mwanamke, ushiriki wa mwanamke kuchangia fikra za siasa na uongozi.

Aliwataka kuchambua na kuangalia mambo yapi yatakayounganisha wanasiasa wote katika kutetea masuala ya kitaifa ikiwa ni pamoja na utu na haki za mwanamke na pia mfumo wa uongozi utakaowezesha vyama vya siasa kuimarisha demokrasia shirikishi yenye mrengo wa jinsia ndani ya vyama.

Pia kuchambua mfumo wa uongozi unaowezesha vyama kutatua migogoro ndani ya vyama vyao bila kutumia vitisho, na hususani vinavyoashiria kumsababisha mwanamke wa Tanzania asipende kushiriki katika shughuili za siasa au anaposhiriki ajisikie yuko salama.

Kwa upande wake Mjumbe wa Wanawake na Katiba/uchaguzi na uongozi, Bi. Laeticia Mukurasi akizungumza katika majadiliano hayo, alisema malengo ni kujadili kwa pamoja umuhimu wa kuzingatia misingi ya usawa wa jinsia katika masuala ya siasa na  uongozi nchini nchini.

Kujenga makubaliano ya pamoja jinsi waandishi wa habari watakavyochechemua umuhimu wa kuzingatia misingi ya jinsia kwenye masuala ya siasa na uongozi katika majukumu yao, na kujengeana uwezo wa masuala ya usawa wa jinsia na uongozi kwa ujumla.






Hivyo makala Mtandao wa Wanawake na Katiba wajadiliana na wahariri Dar

yaani makala yote Mtandao wa Wanawake na Katiba wajadiliana na wahariri Dar Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mtandao wa Wanawake na Katiba wajadiliana na wahariri Dar mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/mtandao-wa-wanawake-na-katiba.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Mtandao wa Wanawake na Katiba wajadiliana na wahariri Dar"

Post a Comment