title : MAKAMU WA RAIS AANZA ZIARA MKONI SIMIYU
kiungo : MAKAMU WA RAIS AANZA ZIARA MKONI SIMIYU
MAKAMU WA RAIS AANZA ZIARA MKONI SIMIYU
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi wa mkoa wa Simiyu kuhakikisha kila shule ya sekondari inayojengwa inajengwa ikiwa na maabara.
Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati akiwahutubia wananchi Lamadi wilaya ya Busega mkoani Simiyu ikiwa siku yake ya kwanza ya ziara ya siku tano mkoani humo.
Makamu wa Rais ambaye alianza ziara yake kwa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa maji uliopo Kiloleli ambapo mradi huo ukikamilika utasaidia kupatikana kwa maji safi na salama kwa vijiji vitatu na utagharimu shilingi za kitanzania bilioni 1.6 ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 80%.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa maji Kiloleli ambao utafaidisha vijiji vitatu, kulia ni Mbunge wa Jimbo la Busega Dkt. Raphael Chegeni.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wananchi wa Masanza Kona, Kiloleli wilaya ya Busega mkoani Simiyu.
Mbunge wa Jimbo la Busega Dkt. Raphaele Chegeni akizungumza mbele ya Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa kusalimia wananchi waliojitokeza kwa wingi barabarani eneo la Nyashimo kumsalimia Makamu wa Rais ambaye ameanza ziara ya siku tano mkoani Simiyu.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba za Viongozi wa Mkoa katika eneo la Nyaumata, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala MAKAMU WA RAIS AANZA ZIARA MKONI SIMIYU
yaani makala yote MAKAMU WA RAIS AANZA ZIARA MKONI SIMIYU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAKAMU WA RAIS AANZA ZIARA MKONI SIMIYU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/makamu-wa-rais-aanza-ziara-mkoni-simiyu.html
0 Response to "MAKAMU WA RAIS AANZA ZIARA MKONI SIMIYU"
Post a Comment