Mahakama ya Afrika kuhamasisha wadau Jamhuri ya Demokrasia ya Kiarabu ya Sahrawi (SADR)

Mahakama ya Afrika kuhamasisha wadau Jamhuri ya Demokrasia ya Kiarabu ya Sahrawi (SADR) - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mahakama ya Afrika kuhamasisha wadau Jamhuri ya Demokrasia ya Kiarabu ya Sahrawi (SADR), tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mahakama ya Afrika kuhamasisha wadau Jamhuri ya Demokrasia ya Kiarabu ya Sahrawi (SADR)
kiungo : Mahakama ya Afrika kuhamasisha wadau Jamhuri ya Demokrasia ya Kiarabu ya Sahrawi (SADR)

soma pia


Mahakama ya Afrika kuhamasisha wadau Jamhuri ya Demokrasia ya Kiarabu ya Sahrawi (SADR)

Arusha, 4 February, 2018-Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR) inaendelea kuimarisha juhudi zake za kuitangaza kwa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika(AU) pamoja na wadau mbalimbali ili waweze kuitumia kikamilifu kupeleka mashauri yaliyotimiza vigezo katika Mahakama hiyo.

Katika kufanikisha juhudi hizo, AfCHPR inafanya ziara ya kikazi katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Kiarabu ya Sahrawi (SADR) ili kukutana na kufanya mazungumzo na wadau mbalimbali.

Katika ziara hiyo inayofanyika kuanzia Februari 05 hadi 07 mwaka huu,wajumbe wa Mahakama hiyo wakiwemo majaji 3 wataendesha semina kwa wadau husika na pia watakutana na Rais wa nchi hiyo pamoja na Spika wa bunge la SADR.

Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu,Jaji Sylvain Ore’,amesema semina hiyo inalenga kukuza uelewa wa wadau hao juu ya uwepo wa Mahakama hiyo hivyo, kuleta hamasa kwa nchi nyingi za Umoja wa Afrika kuridhia itifaki iliyoanzisha AfCHPR na kutoa tamko rasmi la kutambua na kukubali mamlaka ya Mahakama hiyo kuweza kupokea kesi za watu binafsi na Mashirika yasiyo ya kiserikali(NGO’s).

“Ili Mahakama iweze kufanikisha malengo yake na pia kuimarisha mfumo wa haki za Binadamu barani Afrika,nchi nyingi za Umoja wa Afrika hazina budi kuridhia itifaki iliyounda Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na watu kwa mujibu wa kifungu cha 34(6)” alisema Rais huyo wa AfCHPR.

Tangu mwaka 2010,Mahakama hiyo ya Afrika imefanikiwa kuendesha programu mbalimbali zinazolenga kutoa elimu ya uwepo wa Mahakama hiyo pamoja na shughuli zake katika baadhi ya nchi za Afrika ikiwemo Chad,Ethiopia,Afrika ya Kusini,Ghana,Malawi,Kenya,Uganda,Zambia na Ivory Coast.

Mahakama ya Afrika ilianzishwa kwa mujibu wa kifungu namba 1 cha itifaki ya mkataba ulioanzisha Mahakama hiyo ambapo Itifaki hiyo ilikubaliwa Juni 09,1998 nchini Burkina Faso na ikaanza kutumika Januari 25,2004 na ilianza shughuli zake rasmi Novemba 2006.

Aidha hadi Desemba mwaka jana,jumla ya maombi 155 ya mashauri yalipokelewa na Mahakama hiyo na kesi 32 zimekamilishwa.


Hivyo makala Mahakama ya Afrika kuhamasisha wadau Jamhuri ya Demokrasia ya Kiarabu ya Sahrawi (SADR)

yaani makala yote Mahakama ya Afrika kuhamasisha wadau Jamhuri ya Demokrasia ya Kiarabu ya Sahrawi (SADR) Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mahakama ya Afrika kuhamasisha wadau Jamhuri ya Demokrasia ya Kiarabu ya Sahrawi (SADR) mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/mahakama-ya-afrika-kuhamasisha-wadau.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Mahakama ya Afrika kuhamasisha wadau Jamhuri ya Demokrasia ya Kiarabu ya Sahrawi (SADR)"

Post a Comment