title : MAENEO YANAYOTUMIKA KUPITISHA DAWA ZA KULEVYA NCHINI YATAJWA
kiungo : MAENEO YANAYOTUMIKA KUPITISHA DAWA ZA KULEVYA NCHINI YATAJWA
MAENEO YANAYOTUMIKA KUPITISHA DAWA ZA KULEVYA NCHINI YATAJWA
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
SERIKALI imebaini kwamba maeneo ya bandari, bahari kuu,vituo vya mabasi na viwanja vya ndege bado yanatumika kupitisha dawa za kulevya nchini. Hata hivyo imeelezwa kuwa wafanyabiashara, wasambazaji na watumiaji wa dawa za kulevya wameendelea kukamatwa, lengo ni kuhakikisha biashara hiyo inamalizika kabisa.
Hayo yamesemwa leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akikabidhi gari kwa Kamishna Generali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Rogers Siyanga.
Amefafanua mbali na kukamata meli, pia Serikali imewakamata wasambazaji pamoja na kundi kubwa la wafanyabiashara wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya sambamba na watumiaji, lengo ni kuhakikisha Tanzania inakuwa salama na kizazi chenye uwezo wa kuzalisha mali.
"Serikali imepiga hatua kubwa katika vita dhidi ya dawa za kulevya na hivi karibuni imekamata meli nyingi, moja ilikiwa inatokea pwani ya Msumbiji na ilikamatiwa maeneo ya Mtwara ikiwa na dawa nyingi za kulevya.
"Niwakati wa Serikali kuendelea kuiwezesha Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya na leo hii tunawakabidhi gari hili jipya kabisa ili kuendelea na utekelezaji wa majukumu yake ipasavyo.
"Watanzania wenye tabia ya kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya kuacha ikiwa ni pamoja na kazi ya kusambaza, kuzalisha na kutumia na watakaokamatwa wakijihusisha nayo watachukuliwa hatua kali za kisheria,"amesema.
Ameongeza kwa sasa Serikali inajenga maabara ambayo itatumiwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa dawa wanazozikamata.
Waziri Mkuu amesema wananchi wanatakiwa kushirikiana na Serikali katika vita dhidi ya dawa za kulevya kwa kutoa taarifa mara wanapowabaini wafanyabiashara, watumiaji na wasambazaji wa dawa hizo.
Pia wahakikishe wanawalinda vijana ili wasijihusishe na dawa za kulevya. Kwa upande wake Siyanga ameishukuru Serikali kwa kuipatia mamlaka hiyo gari, ambapo alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi waachane na biashara ya dawa za kulevya. Pia amesema jamii iache kuwanyanyapaa watu ambao wameathirika na matumizi ya dawa za kulevya na kushauri kuwa walioathirika na dawa za kulevya wanastahili kupelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu ya huduma za methadone.
Hivyo makala MAENEO YANAYOTUMIKA KUPITISHA DAWA ZA KULEVYA NCHINI YATAJWA
yaani makala yote MAENEO YANAYOTUMIKA KUPITISHA DAWA ZA KULEVYA NCHINI YATAJWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAENEO YANAYOTUMIKA KUPITISHA DAWA ZA KULEVYA NCHINI YATAJWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/maeneo-yanayotumika-kupitisha-dawa-za.html
0 Response to "MAENEO YANAYOTUMIKA KUPITISHA DAWA ZA KULEVYA NCHINI YATAJWA"
Post a Comment