title : LESENI MADUKA KUBADILISHA FEDHA ZA KIGENI KAA LA MOTO
kiungo : LESENI MADUKA KUBADILISHA FEDHA ZA KIGENI KAA LA MOTO
LESENI MADUKA KUBADILISHA FEDHA ZA KIGENI KAA LA MOTO
*Kati ya maduka 297 ya awali sasa yamebaki 70,matawi 40
*BoT yaendelea kuchambua leseni za maduka 65,
Na Said Mwishehe,Blogu ya jamii
BENKI Kuu ya Tanzania(BoT)imesema wakati mchakato wa kutoa upya wa leseni kwa maduka ya kubadilisha fedha za kigeni ukiendelea, maduka yaliyokidhi vigezo hadi sasa ni 71 na matawi 40 kati ya maduka 297 yaliyokuwepo awali.
Juni mwaka jana, wamiliki was maduka hayo walitangaziwa kuwa wanatakiwa kuomba upya leseni za maduka ya kubadilisha fedha na hatua ilitokana na tuhuma mbalimbali za maduka hayo ikiwamo ya kwamba kuna baadhi ya maduka yanatumika katika utakashiji fedha.
Akizungumza mchakato kuhusu utoaji upya wa leseni kwa maduka hayo , Meneja wa Huduma za Fedha na Maduka ya kubadilisha fedha chini ya Usimamizi wa Idara ya Mabenki, Eliamringi Mandari amefafanua watatoa taarifa rasmi kuhusu mchakato huo.
Mandari wakati anatoa mada inayohusu kanuni mpya za usimamizi wa maduka ya fedha kwa waandishi wa habari waliopo kwenye semina iliyoandaliwa na BoT.Lengo la semina hiyo ni kuwajengea uwezo wa taarifa sahihi zinazohusu uchumi,biashara na fedha,ambapo ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa kati ya maduka hayo 297ni maduka 71 tu ndio yamekidhi vigezo.
"Naomba hapa tuelewane kwanza,mchakato wa kutoa leseni kwa maduka hayo ya kubadilisha fedha za kigeni bado unaendelea na utakamilika siku za karibuni na baada ya hapo tutatoa taarifa rasmi."Hii ambayo tunaeleza si kwamba ndio taarifa ya mwisho ila naelezea hatua ambayo tumefikia hadi sasa.Mchakato huo ulianza Juni mwaka jana na ulitakiwa kukamilika Desemba mwaka jana.
Hivyo makala LESENI MADUKA KUBADILISHA FEDHA ZA KIGENI KAA LA MOTO
yaani makala yote LESENI MADUKA KUBADILISHA FEDHA ZA KIGENI KAA LA MOTO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala LESENI MADUKA KUBADILISHA FEDHA ZA KIGENI KAA LA MOTO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/leseni-maduka-kubadilisha-fedha-za.html
0 Response to "LESENI MADUKA KUBADILISHA FEDHA ZA KIGENI KAA LA MOTO"
Post a Comment