KANALI NDAGALA AHIMIZA WAMILIKI SHULE BINAFSI KUTOA ELIMU ILIYO BORA

KANALI NDAGALA AHIMIZA WAMILIKI SHULE BINAFSI KUTOA ELIMU ILIYO BORA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KANALI NDAGALA AHIMIZA WAMILIKI SHULE BINAFSI KUTOA ELIMU ILIYO BORA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KANALI NDAGALA AHIMIZA WAMILIKI SHULE BINAFSI KUTOA ELIMU ILIYO BORA
kiungo : KANALI NDAGALA AHIMIZA WAMILIKI SHULE BINAFSI KUTOA ELIMU ILIYO BORA

soma pia


KANALI NDAGALA AHIMIZA WAMILIKI SHULE BINAFSI KUTOA ELIMU ILIYO BORA


Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

MKUU wa Wilaya ya Kakonko, Kanali Hosea Ndagala  amewataka wamiliki wa shule binafsi zinazoanzishwa wilayani humo kuhakikisha wanatoa elimu iliyo bora na kujikita katika masomo ya sayansi.

Amefafanua kwa sasa nchi ya Tanzania inaingia katika ychumi wa Vlviwanda na kuwasaidia vijana hao wapate ajira kwa urahisi.

Kanali Ndagala aliyasema jana(juzi) wilayani Kakonko wakati wa uzinduzi wa Shule ya Sekondari ya Berea iliyoko wilayani humo ambapo aliwataka wamiliki kutafuta walimu wenye uwezo wa kufundisha masomo ya sanyansi.

"Lengo la kujikita kwenye masomo ya sayansi ni kupata wataalamu wa viwanda vitakavyo anzishwa kwakua mpango wa Serikali ni kuifikisha nchi katika uchumi wa viwanda na nilazima wazingatie utoaji wa elimu iliyo bora," amesema.Aidha amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii na kuwa wasilizike na kumaliza elimu ya kidato cha nne, kwani huo ni msingi tu unao fungua maisha yao.

Pia kuhakikisha wanatumia fursa hiyo ya kuwekewa shule karibu kusoma kwa bidii na kuweza kufika mbali ilikuweza kuinua Wilaya ya Kakonko nayo kuwa na viwanda na wataalamu walio elimika.

Hata hivyo amewaomba wananchi wa wilaya hiyo kuwa wazalendo kwa kuwaunga mkono wale wote wanaoanzisha shule kwa kuwapeleka watoto waweze kupata elimu, na kuacha kuwakatisha tamaa wale wato wanaotaka kuwekeza, kwa maneno ya kejeri hali hiyo inapelekea Wilaya hiyo kushindwa kuinuka kiuchumi kwani wawekezaji ndio chachu ya maendeleo katika Wilaya.

"Niwatie moyo wote mnaotaka kuwekeza katika Wilaya hii, Serikali ipo kwa ajili ya kuwatia moyo, na Serikali inahitaji wawekezaji."Nikupongeze mmiliki wa shule hii kwani najua umepitia changamoto nyingi umepitia lakini hukukata tamaa umekuwa mzalendo kuja kuwekeza nyumbani.

"Changamoto zilizopo zifanye kuwa fursa ili tuweze kuhakikisha wilaya yetu inainuka katika elimu na uchumi kwa ujumla", alisema Kanal Ndagala.Kwa upande wake Mkurugenzi wa shule ya Berea Baraka Mathias alisema anaishukuru Serikali kwa ushirikiano aliopata ikiwa ni pamoja na  kupatiwa usajili wa shule hiyo.

Ameomba wananchi kuacha tabia ya kuwavunja moyo wale wote wenye nia ya kuinua Wilaya ya Kakonko kwa kuleta maendeleo.Pia amewataka vijana kusimamia malengo yao na ndoto walizonazo kuziishi ili kufanikisha mipango yao na kuwaomba wawekezaji wengine kuja kuwekeza Katika wilaya hiyo ambayo imesahaulika ilikuweza kufungua fursa na kusaidia kuinua uchumi wa Wanakakonko.

Amesema shule hiyo inajumla ya wanafunzi 103 na ni moja kati ya shule zilizo fanya vizuri wilayani humo, pamoja na changamoto zote hakukata tamaa .Amefafanua amehakikisha anasimamia wazo lake la kuanzisha shula katika  wilaya hiyo na wanafunzi wapate elimu kwa ukaribu zaidi. 
Mkuu wa wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala akikata utepe kufungua shule ya Sekondari Berea
Mkuu wa wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala akizungumza wakati wa kufungua shule ya Sekondari Berea -


Hivyo makala KANALI NDAGALA AHIMIZA WAMILIKI SHULE BINAFSI KUTOA ELIMU ILIYO BORA

yaani makala yote KANALI NDAGALA AHIMIZA WAMILIKI SHULE BINAFSI KUTOA ELIMU ILIYO BORA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KANALI NDAGALA AHIMIZA WAMILIKI SHULE BINAFSI KUTOA ELIMU ILIYO BORA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/kanali-ndagala-ahimiza-wamiliki-shule.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "KANALI NDAGALA AHIMIZA WAMILIKI SHULE BINAFSI KUTOA ELIMU ILIYO BORA"

Post a Comment