Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu aongea na wanahabari

Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu aongea na wanahabari - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu aongea na wanahabari, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu aongea na wanahabari
kiungo : Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu aongea na wanahabari

soma pia


Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu aongea na wanahabari

Na Ali Issa - MAELEZO 
Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu  amesema uwendeshaji wa kesi kwa mwaka uliomaliza haukuwa mbaya na kwamba  kiasi Idara ya Mahakama imefanikiwa katika utekeleza wa majukumu yake.
Hayo ameyasema leo huko Afisini kwake Vuga  mjini Zanzibar wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuelekea maazimisho ya wa wiki ya sheria duniani ambayo kilele chake hufanyika February 12 ya kila mwaka. Amesema pamoja na changa moto zinazoikabili Idara ya Mahakama lakini wamefanikiwa kuzitolea hukumu kesi mbalimbali ikiwemo za udhalilishaji na Madawa ya kulevya nchini
Amesema licha ya Wananchi wengi kulalamikia Idara hiyo kwa kushindwa kutoa hukumu kama wanavyodai lakini changamoto kubwa inayojitokeza ni kushindwa kutoa mashirikiano ipasavyo hasa katika kutoa ushahidi. Jaji Makungu amesema ni vyema Wananchi kutoa mashirikiano ipasavyo ikiwemo kutoa ushahidi kila inavyohitajika ili kuwatia hatiani wale wanaofanya makosa na jinai mbalimbali nchini.
“Huwezi kumtia mtu hatiani bila kutolewa ushahidi wa kutosha..Wananchi wengi wanashindwa kutoa ushahidi” Alisema Jaji Mkuu Makungu. Akielezea mafanikio amesema Mahakama imefanikiwa kuyakarabati Majengo yao na kuwa katika hali bora na hivyo kuwarahisishia Watendaji wa mahakama kuwajibika vizuri.
Aidha alisema wameweza  kuweka vizuri Maktaba yao hali ambayo inawejengea uwezo Wanasheria kwa kupata taluma na miongozo ya kazi kupitia Maktaba hiyo.
Akizungumzaia kuhusu shamra shamra za maadhimisho hayo Jaji Makungu amesema wanatarajia kufanya maonesho ya siku tatu kuazia February 9 hadi 11 katika viwanja vya maisara. Jaji Makungu alisema  kilele cha sherehe hizo zitafanyika baraza la wakilishi la zamani na mgeni rasmi wanatarajia atakuwa DKT. Ali muhamed shein na Ujumbe wa mwaka huu ni kuimarisha utwala wa sheria na uchumi .
Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe,Omar Othman Makungu katikati akizungumza na Waandishi wa Habari   kuhusiana na Siku ya Sheria Duniani ambapo kwa Zanzibar kitafanyika kilele chake 12-02-2018 katika bustani ya Victoria Mnazi mmoja mjini Unguja. Ujumbe wa mwaka huu ni Kuimarisha Utawala wa Sheria na Kuimarisha Uchumi Zanzibar.kulia yake ni Kaimu mrajisi wa Mahkama Yessaya Kayange na kushoto ni Hakimu wa Mahkama ya Watoto Sabra Ali Mohammed.
 Sehemu ya Waandishi wa Habari waliohudhuria  Mkutano wa Jaji Mkuu wa Zanzibar Mh,Omar Othman Makungu akielezea kuhusiana na Siku ya Sheria Duniani ambapo kwa Zanzibar kitafanyika kilele chake 12-02-2018 katika bustani ya Victoria Mnazi mmoja mjini Unguja.Ujumbe wa mwaka huu ni Kuimarisha Utawala wa Sheria na Kuimarisha Uchumi Zanzibar.

Kaimu Mrajisi wa Mahkama  Yessaya Kayange akitolea ufafanuzi wa baadhi ya maswali yalioulizwa katika  Mkutano wa Jaji Mkuu wa Zanzibar Mh,Omar Othman Makungu akielezea kuhusiana na Siku ya Sheria Duniani ambapo kwa Zanzibar kitafanyika kilele chake 12-02-2018 katika bustani ya Victoria Mnazi mmoja mjini Unguja.Ujumbe wa mwaka huu ni Kuimarisha Utawala wa Sheria na Kuimarisha Uchumi Zanzibar.kushoto ni Hakimu wa Mahkama ya Ardhi Said Hemed.


Hivyo makala Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu aongea na wanahabari

yaani makala yote Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu aongea na wanahabari Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu aongea na wanahabari mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/jaji-mkuu-wa-zanzibar-omar-othman.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu aongea na wanahabari"

Post a Comment