title : BoT YAELEZEA UMUHIMU VYOMBO VYA HABARI KUFIKIA UCHUMI WA VIWANDA
kiungo : BoT YAELEZEA UMUHIMU VYOMBO VYA HABARI KUFIKIA UCHUMI WA VIWANDA
BoT YAELEZEA UMUHIMU VYOMBO VYA HABARI KUFIKIA UCHUMI WA VIWANDA
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
BENKI Kuu ya Tanzania(BoT), imesema vyombo vya habari nchini mchango wao ni muhimu zaidi ili kufikia azma ya uchumi wa viwanda huku ikisisitiza haja ya kuandikwa taarifa sahihi zinazohusu masuala ya chumi, fedha na biashara.
Hayo yamesemwa leo mkoani Mtwara na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT),upande wa Utawala na Udhibiti wa Ndani, Julian Banzi wakati anafungua rasmi Semina kwa waandishi wa habari yenye lengo la kuwajengea uwezo katika kuandika na kuchambua masuala ya uchumi, biashara na fedha.
"Nafasi yenu ni muhimu, hivyo muitumie kwa ajili ya kusaidia nchi yetu.Ni vizuri badala ya kutumia muda mwingi kuandika mambo ambayo hayana uhusiano na uchumi, sasa mkajikita kutumia muda wenu mwingi kuandika mambo yanayohusu uchumi."Ujenzi wa reli unaendelea ni vema waandishi wakaandika,kuna mradi wa bomba la mafuta ni vema vyombo vya habari vikaandika.Kwa kupitia vyombo vya habari tunaamini wananchi watapata taarifa sahihi ya maendeleo yanayoendelea kufanyika nchini,"amesema Banzi.
Amefafanua BoT inafuatilia kwa karibu makala mbalimbali zinazohusu uchumi na hilo ni jambo jema kuendelea kufanywa na vyombo vya habari na ikiwezekana muda wa kuzungumzia masuala yanayohusu uchumi uongezeke zaidi.Banzi amesema wananchi wanahitaji kupata taarifa sahihi zinazohusu uchumi, hivyo ni jukumu la waandishi wa habari na vyombo vyao kuhakikisha wanatoa taarifa sahihi ambazo hazitakuwa za upotoshaji.
"Mtakapoandika taarifa sahihi zinazohusu uchumi na majukumu ya BoT mtasaidia kupunguza maswali ambayo wakati mwingine wananchi wanajiuliza,"amesema Banzi.Ametoa mfano wapo watu ambao kazi yao nikukaa vijiweni na kujadili uchumi wakati wenyewe wanashindwa kuchangia kwenye huo uchumi.
"Wanakaa vijiweni na kisha wanauliza kama uchumi umepanda mbona mifukoni hakuna kitu.Ni jukumu la vyombo vya habari kuendelea kutoa taarifa zitakazohamasisha wananchi kushiriki kwenye maendeleo ya uchumi kwa kufanya kazi badala ya kukaa vijiweni wakilalamika,"amesema Banzi.
Amesisitiza ni vema vyombo vya habari vikaajenga matumaini kwa wananchi ili washiriki kwenye kuleta mandeleo nchini."Ombi letu ni kuona vyombo vya habari vinaandika makala nyingi kuhusu uchumi,biashara na fedha".Kuhusu semina hiyo,Banzi amesema BoT imedhamiria kuwajengea uwezo waandishi wa habari na sababu kubwa ni kuona taarifa ambazo zinaandikwa zinakuwa sahihi.
"Kupitia semina hii mtajifunza majukumu mbalimbali ya BoT.Najua mtajifunza mambo mengi na mbali ya mafunzo mtapata nafasi ya kufanya ziara kwenye maeneo ya kiuchumi mkoani Mtwara.Mtakwenda maeneo ya kuchaka gesi kwani hilo nalo ni eneo muhimu la kiuchumi,"amesema Banzi.Banzi ametoa angalizo kuwa pamoja na kuwepo kwa taarifa sahihi ambazo zinahusu uchumi bado kuna baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikitoa taarifa za kupotosha na matokeo yake BoT inalazimika kutumia nguvu nyingi kuzungumzia taarifa sahihi.
"Kuna wakati zinaandikwa habari ambazo zinakatisha tamaa kutokana na kuendelea kwa taarifa za uchokozi BoT tutaendelea kuwaelimisha waandishi wa habari,"amesema.
Hivyo makala BoT YAELEZEA UMUHIMU VYOMBO VYA HABARI KUFIKIA UCHUMI WA VIWANDA
yaani makala yote BoT YAELEZEA UMUHIMU VYOMBO VYA HABARI KUFIKIA UCHUMI WA VIWANDA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BoT YAELEZEA UMUHIMU VYOMBO VYA HABARI KUFIKIA UCHUMI WA VIWANDA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/bot-yaelezea-umuhimu-vyombo-vya-habari.html
0 Response to "BoT YAELEZEA UMUHIMU VYOMBO VYA HABARI KUFIKIA UCHUMI WA VIWANDA"
Post a Comment