title : BIL.1.7 KUJENGA MIUNDOMBINU YA ELIMU SIMIYU
kiungo : BIL.1.7 KUJENGA MIUNDOMBINU YA ELIMU SIMIYU
BIL.1.7 KUJENGA MIUNDOMBINU YA ELIMU SIMIYU
Uwekezaji katika sekta ya elimu Nchini kupitia mpango wa kuinua ubora wa elimu (EQUIP-Tanzania) ambao umelenga kuboresha mchakato wa kufundisha na matokeo ya kujifunza kwa watoto nchini umeweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa Mkoani Simiyu.
Uwekezaji huo ambao unafadhiliwa na serikali ya Uingereza kupitia Wizara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (DFID) umeleta ufanisi wa elimu na kufanya viwango cha ufaulu kuwa juu kutoka asilimia 36 mwaka 2013 mpaka asilimia 68 2017.
Na katika kutimiza hayo Jumla ya kiasi cha shilingi Bil 1.7 kutoka DFID kupitia mradi wa kuinua ubora wa Elimu Nchini (Equip) zimetolewa kwa Serikali ya Mkoani Simiyu kwa ajili ya kujenga na kuboresha miundombinu ya elimu Mkoani humo .
Akizungumzia nia ya serikali ya Uingereza wakati wa mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan , Mkuu wa DFID-Tanzania Elizabeth Arthy alisema wametoa kiasi hicho cha fedha kwa serikali ya Mkoa wa Simiyu ili kuhakikisha wanatatua changamoto ya miundombinu iliyopo.
Arthy alisema kuwa kiasi hicho cha fedha ambacho kinatarajiwa kutumika katika kuboresha miundombinu hiyo na kujenga vyumba vya madarasa, ofisi za walimu pamoja matundu ya vyoo kitasaidia kwa kiasi kikubwa kuleta ufanisi wa utoaji elimu kwa walimu na wanafunzi.
Mkuu huyo alieleza kuwa tangu shirika lake lianze kusaidia katika Elimu ,Mkoa wa Simiyu umeweza kupata mafanikio makubwa na ya haraka ambayo yamesaidia kuuweka Mkoa katika nafasi nzuri Kitaifa katika matokeo ya mitihani ya kuhitimu elimu ya Msingi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka aliuelezea mpango wa kuinua ubora wa elimu Tanzania kwa Mkoa wake kuwa ni mpango ambao umeweza kuleta mabadiliko makubwa ya kukuza viwango vya ufaulu wa wanafunzi.
Mtaka anaeleza wanalishukuru shirika la maendeleo ya uingereza (DFID) kupitia mpango wa kuinua ubora wa elimu kwa kuona kuwa Tanzania na Mkoa wake unahitaji msaada huo wa kuinua kiwango cha ufaulu pamoja na uboreshaji wa mazingira ya elimu.
Amesema kupitia msaada huo wa fedha kiasi cha shilingi Bil 1.7 zilizotolewa kwao na shirika la DFID kwa mwaka huu za kuboresha mazingira ya elimu ,zitawasaidia kujenga vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo ambavyo vyote hivyo ni changamoto kubwa Mkoani kwake.
Anaongeza kuwa kupitia fedha hizo anaanimi tatizo la uhaba wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo utapungua kwa kiasi kikubwa na kwamba atasimamia vema fedha hizo ili ziweze kutumika ipasavyo.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mheshimiwa Anthony Mtaka akimuelezea Makamu wa Raisi utekelezaji wa mpango wa EQUIP-Tanzania mkoani Simiyu.
Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza nchini Tanzania Bibi Elizabeth Arthy akizungumza mbele ya makamu wa Rais juu ya mchango wa serikali ya Uingereza katika kuboresha elimu.
Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza nchini Tanzania Bibi Elizabeth Arthy akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa shule ya msingi Gamondo A iliyoo wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Bibi Elizabeth Arthy alipotembelea shule ya msingi Gamondo A mkoani Simyu, kuona utekelezaji wa mpango wa EQUIP-Tanzania.
Hivyo makala BIL.1.7 KUJENGA MIUNDOMBINU YA ELIMU SIMIYU
yaani makala yote BIL.1.7 KUJENGA MIUNDOMBINU YA ELIMU SIMIYU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BIL.1.7 KUJENGA MIUNDOMBINU YA ELIMU SIMIYU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/bil17-kujenga-miundombinu-ya-elimu.html
0 Response to "BIL.1.7 KUJENGA MIUNDOMBINU YA ELIMU SIMIYU"
Post a Comment