title : Heroes Ikiifunga Kesho itatinga nusu fainali kwa kishindo
kiungo : Heroes Ikiifunga Kesho itatinga nusu fainali kwa kishindo
Heroes Ikiifunga Kesho itatinga nusu fainali kwa kishindo
Kikosi cha Zanzibar Heroes kilichoanza dhidi ya Kilimanjaro Stars
Na Abubakar Khatib Kisandu, Machakos Kenya.
Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) ndio kinara wa kundi lao A wakiwa na alama sita katikaMashindano ya kuwania ubingwa wa Kombe la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA SENIOR CHALLENGECUP) Mashindano ambayo yanaendelea nchini Kenya.
Mchezo wa awali Zanzibar Heroes iliichapa Rwanda mabao 3-1 kwa magoli yalofungwa na Mudathir Yahya, Mohd Issa (Banka) na Kassim Suleiman huku mchezo wa pili jana waliifunga Tanzania bara (Kilimanjaro Stars) mabao 2-1 kwa msaada wa mabao yalofungwa na Kassim Suleiman na Ibrahim Hamad Hilika ambapo kesho Jumamosi watacheza mchezo wa tatu dhidi ya wenyeji Kenya.
Endapo kesho Heroes wakifanikiwa kuwafunga Kenya watajihakikishia kutinga hatua ya nusu fainali kwani watafikisha alama 9, alama ambazo hazitoweza kufikiwa na timu yoyote katika kundi hilo.
Katika Mashindano ya mwaka huu Heroes inaonekana kuwavutia wapenzi wengi kutokana na soka safi wanalolitandaza na kuonyesha vipaji walivyonavyo, jambo ambalo limepelekea Wakenya wengi hapa Mjini Machakos kusema kuwa timu yao wanayoipenda ni Zanzibar.
Hivyo makala Heroes Ikiifunga Kesho itatinga nusu fainali kwa kishindo
yaani makala yote Heroes Ikiifunga Kesho itatinga nusu fainali kwa kishindo Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Heroes Ikiifunga Kesho itatinga nusu fainali kwa kishindo mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/heroes-ikiifunga-kesho-itatinga-nusu.html
0 Response to "Heroes Ikiifunga Kesho itatinga nusu fainali kwa kishindo"
Post a Comment