title : AZAM FC, SIMBA SC VITANI KESHO UWANJA WA TAIFA
kiungo : AZAM FC, SIMBA SC VITANI KESHO UWANJA WA TAIFA
AZAM FC, SIMBA SC VITANI KESHO UWANJA WA TAIFA
Na Agness Francis, Globu ya jamii
MABINGWA Afrika Mashariki na kati Azam FC watakuwa wageni dhidi ya vinara aa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba Sc katika mchezo wao wa 2 mzunguko wa 2.
Mchezo huo utakaorindima kesho katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni.
Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi zao Mzizima jijini Dar es Salaam, Msemaji Mkuu wa Azam FC Jaffary Iddy Maganga amesema wapo vizuri katika kumkabili mnyama Simba na kuhakikisha wanaondoka na ushindi wa maboa ili kuweza kuwasogelea vinara hao wenye pointi 38.
Wakati Azam FC wakiwa nyuma kwa pointi 33 wakiwazidi Yanga SC wenye alama 31.
"Tunajua ni mchezo utakaokuwa mgumu dhidi ya Simba SC kwa kuwa wana kikosi kipana na kizuri ila sisi tumejipanga kuhakikisha tunarudi na ushindi nyumbani na vijana wapo vizuri wote wana morari ya kufanya vizuri katika mchezo huo "amesema Jaffary Maganga.
Aidha amesema katika mchezo huo wa vuta ni kuvute dhidi ya wekundu hao wa Msimbazi wataendelea kuwakosa wachezaji wao ambao wapo majerui, Waziri Junior na Joseph Kimwaga ambaye bado hayupo vizuri mpaka sasa kwa kuwa alifanyiwa upasuwaji wa goti hapo siku za nyuma..
"Mchezaji wetu Aboubakar Salum maarufu kama (Sure boy) atarejea mchezoni Kesho akiwa amemalizia kutumikia adhabu yake ya kupewa kadi nyekundu katika mchezo wa 16 wa kukamilisha mzunguko wa 1 uliochezwa pale Chamazi na Mabingwa watetezi YangaSC na kusababisha kukosa mechi iliyopita dhidi ya NdandaFC," amesema Maganga.
Msemaji Mkuu AzamFc, Jaffary Iddy Maganga akizungumza na waandishi wa habari leo katika Ofisi zao Mzizima Jijini Dar es Salaam, kuhusu maandalizi yanayoendelea katika kikosi chake ambapo kesho watavaana na mnyama simba katika Dimba la Uwanja wa Taifa majira ya saa 10 jioni.
Hivyo makala AZAM FC, SIMBA SC VITANI KESHO UWANJA WA TAIFA
yaani makala yote AZAM FC, SIMBA SC VITANI KESHO UWANJA WA TAIFA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala AZAM FC, SIMBA SC VITANI KESHO UWANJA WA TAIFA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/azam-fc-simba-sc-vitani-kesho-uwanja-wa.html
0 Response to "AZAM FC, SIMBA SC VITANI KESHO UWANJA WA TAIFA"
Post a Comment