ZOEZI LA UPIGAJI CHAPA MIFUGO LAONGEZEWA MUDA WA MWEZI MMOJA.

ZOEZI LA UPIGAJI CHAPA MIFUGO LAONGEZEWA MUDA WA MWEZI MMOJA. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa ZOEZI LA UPIGAJI CHAPA MIFUGO LAONGEZEWA MUDA WA MWEZI MMOJA., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : ZOEZI LA UPIGAJI CHAPA MIFUGO LAONGEZEWA MUDA WA MWEZI MMOJA.
kiungo : ZOEZI LA UPIGAJI CHAPA MIFUGO LAONGEZEWA MUDA WA MWEZI MMOJA.

soma pia


ZOEZI LA UPIGAJI CHAPA MIFUGO LAONGEZEWA MUDA WA MWEZI MMOJA.

Mwambawahabari

Na Stella Kalinga, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina ameongeza muda wa mwezi mmoja kwa Halmashauri hapa nchini kukamilisha zoezi la upigaji chapa mifugo na kuwataka watendaji wote wa Serikali wanaohusika kuhakikisha mifugo yote inapigwa chapa.
Waziri Mpina ameyasema hayo wakati wa kuhitimisha zoezi la upigaji chapa Kitaifa katika Kijiji cha Migato wilaya ya Itilima mkoani Simiyu, zoezi ambalo lilianza rasmi Kitaifa mwezi Desemba, 2016 na kupangwa kukamilika Desemba 31, 2017.
“Kwa kuwa hadi sasa zoezi hili limetekelezwa kwa asilimia 38.5 kutokana na sababu mbalimbali, Mimi Luhaga Mpina Waziri wa Mifugo na Uvuvi kwa Mamlaka niliyopewa chini ya sheria ya Utambuzi, Usajili na ufuatiliaji wa mifugo ya mwaka 2010 na kanuni yake, ninaongeza muda wa kupiga chapa mifugo kutoka tarehe 01/01/ 2018 hadi 31/01/2018”alisititiza.
Mpina amesema miongoni mwa changamoto zilizopelekea Halmashauri nyingi kushindwa kutekeleza zoezi hilo kwa asilimia 100 ni baadhi ya halmashauri kutokutenga fedha kwa ajili ya zoezi hilo, kubaini mifugo kutoka nje ya nchi, baadhi ya wafugaji kushindwa kutaja idadi halisi ya mifugo yao na baadhi ya Halmashauri kuwatoza wafugaji zaidi ya shilingi 500 ambayo ndiyo bei elekezi, ambapo ameagiza wafugaji hao waliotozwa zaidi ya shilingi 500 warejeshewe fedha zao.
Ameongeza kuwa hadi kufikia Desemba 31, 2017  Halmashauri 30 hapa nchini hazijapiga kabisa chapa mifugo, halmashauri 23 zimeendesha zoezi hilo chini ya asilimia 10 na akaongeza kuwa orodha ya majina ya viongozi wa wilaya hizo walioshindwa kutekeleza agizo hilo la Serikali ameyawasilisha kwa Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa.
“Halmashauri 30 ambazo hazijapiga chapa kabisa hata ng’ombe mmoja na zile 23 ambazo zimepiga chini ya asilimia 10 majina  ya viongozi wote na Halmashauri husika nimekabidhi orodha hiyo kwa Waziri Mkuu, hatuwezi kuendekeza ukaidi wa maagizo ya Viongozi Wakuu wa Nchi” alisema Mpina.
Akiwasilisha taarifa ya zoezi la Upigaji Chapa katika Mkoa wa Simiyu, Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa, Ndg.Elias Kasuka amesema zoezi hilo mkoani humo lilianza rasmi mwezi Aprili 2017 ambapo hadi sasa ng’ombe zaidi ya 764, 933 wameshapigwa chapa kati ya ng’ombe 1,500,000.
Akitoa maoni yake baada ya kuhitimisha zoezi la upigaji chapa mifugo, Paulo Mabula mfugaji kutoka Migato Itilima amesema wafugaji wamelipokea kwa furaha agizo la Waziri wa Mifugo na Uvuvi kuongeza siku za kwa ajili ya kupiga chapa kwani litawasaidia wafugaji ambao bado hawajakamilisha ili kuondokana na changamoto ya wizi wa mifugo.
Naye Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Itilima, Mhe.Mahamoud Mabula amemuomba Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe.Luhaga Mpina kuwasaidia wafugaji wa Wilaya hiyo na maeneo mengine ya Mkoa huo kufanya vikao vya ujirani mwema na wale wa mikoa jirani ili kujadiliana namna ya kuondoa changamoto ya wizi wa mifugo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe.Benson Kilangi amesema viongozi na wataalam wa wilaya hiyo wamekuwa wakiwahamasisha wafugaji kupanga matumizi bora ya ardhi ili waweze kutenga maeneo kwa ajili ya malisho na kuyawekea miundombinu muhimu kwa ajili ya mifugo ikiwemo maji, majosho pamoja malisho.


Hivyo makala ZOEZI LA UPIGAJI CHAPA MIFUGO LAONGEZEWA MUDA WA MWEZI MMOJA.

yaani makala yote ZOEZI LA UPIGAJI CHAPA MIFUGO LAONGEZEWA MUDA WA MWEZI MMOJA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala ZOEZI LA UPIGAJI CHAPA MIFUGO LAONGEZEWA MUDA WA MWEZI MMOJA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/zoezi-la-upigaji-chapa-mifugo_1.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "ZOEZI LA UPIGAJI CHAPA MIFUGO LAONGEZEWA MUDA WA MWEZI MMOJA."

Post a Comment