title : YANGA ,MWADUI FC KUVAANA KESHO UWANJA WA UHURU
kiungo : YANGA ,MWADUI FC KUVAANA KESHO UWANJA WA UHURU
YANGA ,MWADUI FC KUVAANA KESHO UWANJA WA UHURU
Na Agness Francis-Globu ya jamii
TIMU Soka ya Yanga inatarajia kushuka dimbani kesho kuvaana na timu ya Mwadui Fc katika mchezo wa raundi ya 13 ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Vodavom Tanzania Bara.
Mchezo huo utachezwa saa 10 jioni Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam maarufu la Shamba la Bibi.Katika mechi ya raundi ya 12 Yanga walipoteza mchezo wao dhidi ya Mbao FC uliochezwa jijini Mwanza katika Uwanja wa CCM Kirumba
Mabingwa hao watetezi watashuka dimbani huku wakimkosa mshambuliaji wake wa kimataifa kutoka nchini Zambia Obrey Chirwa aliyefungiwa mechi tatu na Kamati ya Nidhamu ya TFF. Pia watamkosa mshambuliaji wao kutoka Zimbabwe Donard Ngoma ambaye bado hajawa fiti.
Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga Boniphace Mkwasa amesema maandalizi ni mazuri na wanajua mchezo huo utakuwa mgumu.
“Tumejipanga kupambana kuhakikisha tunashinda mchezo wetu wa kesho,” amesisitiza Mkwasa.
Hivyo makala YANGA ,MWADUI FC KUVAANA KESHO UWANJA WA UHURU
yaani makala yote YANGA ,MWADUI FC KUVAANA KESHO UWANJA WA UHURU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala YANGA ,MWADUI FC KUVAANA KESHO UWANJA WA UHURU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/yanga-mwadui-fc-kuvaana-kesho-uwanja-wa_16.html
0 Response to "YANGA ,MWADUI FC KUVAANA KESHO UWANJA WA UHURU"
Post a Comment