title : Wingi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza wapelekea kuanzishwa shule mpya
kiungo : Wingi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza wapelekea kuanzishwa shule mpya
Wingi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza wapelekea kuanzishwa shule mpya
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo ameishauri Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi kuona namna ya kuanzisha shule mpya ili kuleta uwiano wa waalimu katika shule hizo unaoendana na idadi ya wanafunzi ambao wanatarajiwa kuongezeka kila mwaka mpya wa masomo. Ameyasema hayo aliposhiriki kwenye songambele ya ujenzi wa madarasa nane ya Shule ya Sekondari Kirando yanayotarajiwa kutumiwa na wanafunzi 422 waliofaulu kuingia kidato cha kwanza kwa mwaka 2018 katika shule hiyo inayobeba wanafunzi kutoka katika kata mbili zilizopo wilayani Nkasi.
“tunapoangalia kutatua changamoto ya shule hii ya Kirando tuangalie ufumbuzi wa kudumu zaidi, muangalie uwezekano wa kujenga shule nyingine, huo ndio utakuwa ufumbuzi, shule hii ina O – level na A – level, sasa kama kutakuwa na shule nyingine ya O – level peke yake na hii mkaipunguzia mzigo wa kuchukua wanafunzi wengi na walimu wengi katika shule moja”
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo akishiriki kwenye Songambele ya Ujenzi wa madarasa nane katika Shule ya Sekondari Kirando iliyopo Wilayani Nkasi kwaajili ya kutayarisha mazingira kwa wananfunzi 422 wa Kidato cha kwanza kuanza masomo yao Januari 2018.
Ametoa rai kuwa kwa eneo la ekari 60 linalomilikiwa na shule hiyo ya Sekondari Kirando inawezekana kugawa walau ekari 20 kwa shule hiyo mpya jambo litakalowapelekea kupewa waalimu wapya kwa shule mpya na kuleta uwiano wa waalimu kuliko hali ilivyo sasa.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Said Mtanda aliyapokea maagizo hayo na kuahidi kuyafanyia kazi kuanzia ngazi ya Kijiji hadi ngazi ya halmashauri ya Wilaya na kuongeza kuwa suala hilo litawekwa katika bajeti ya mwaka 2018/2019 na kuongeza kuwa wananfunzi wote waliofaulu kuingia kidato cha kwanza watasoma.
Mkuu wa Mkoa wa Wilaya ya Nkasi, Said Mtanda (track ya bluu) akishiriki pamoja na wananchi wa kijiji cha Kirando kwenye Songambele ya Ujenzi wa madarasa nane katika Shule ya Sekondari Kirando iliyopo Wilayani Nkasi kwaajili ya kutayarisha mazingira kwa wananfunzi 422 wa Kidato cha kwanza kuanza masomo yao Januari 2018.
“wanafunzi waliofaulu kuingia kidato cha kwanza katika shule hii ya Kirando ni 422 na tumekubaliana kuwa hadi kufungua shule wananfunzi wote hao wanatakiwa wawe madarasani, lakini tumekubaliana na wazazi kuwa kama serikali tutanunua meza zote 422, lakini tumewahamasisha kuchangia walau mchango wa kiti ili mwanafunzi anapokuja akute meza na kiti ili tulimalize jambo hilo,”
Awali Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari kirando, Erneo Mgina akitoa taarifa fupi ya shule hiyo alisema kuwa shule ina wanafunzi 677 na kutaraji kupokea wanafunzi 422 na upungufu wa madara nane ambayo matatu tayari na mengine yapo katika hatua ya msingi na kutaraji kurekebisha vyumba vitatu vya maabara ili kuwahifadhi wanafunzi kwa muda hadi madarasa yatakapokamilika.
Hili limekuja ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri wa Nchi OR – TAMISEMI kuitaka mikoa iliyokuwa na idadi kubwa ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2018 ukiwemo mkoa wa Rukwa kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanapata madarasa ya kusomea, madawati na vyoo pale shule zitakapofunguliwa tarehe 8/1/2018.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo akitoa maelekezo ya kufanya kazi hiyo ya Songambele muda mfupi kabla ya kuanza kwa kazi hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Wilaya ya Nkasi, Said Mtanda (track ya bluu) akishiriki na baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kirando kubeba jiwe kwaajili ya kuendeleza msingi wa madarasa matatu yanayoendelea kujengwa.
Baadhi wa wananchi wa kijiji cha Kirando wakisaidia kuweka kenchi kwenye moja ya madarasa yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi wa kijiji hicho kwaajili ya maandalizi ya watoto wao waliofaulu kuingia kidato cha kwanza kuanza masomo mwaka 2018 kupata sehemu za kusomea.
Hivyo makala Wingi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza wapelekea kuanzishwa shule mpya
yaani makala yote Wingi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza wapelekea kuanzishwa shule mpya Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Wingi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza wapelekea kuanzishwa shule mpya mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/wingi-wa-wanafunzi-wa-kidato-cha-kwanza.html
0 Response to "Wingi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza wapelekea kuanzishwa shule mpya"
Post a Comment