WAZIRI WA AFYA AKIRI CHANGAMOTO YA UHABA WA MADAKTARI

WAZIRI WA AFYA AKIRI CHANGAMOTO YA UHABA WA MADAKTARI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI WA AFYA AKIRI CHANGAMOTO YA UHABA WA MADAKTARI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI WA AFYA AKIRI CHANGAMOTO YA UHABA WA MADAKTARI
kiungo : WAZIRI WA AFYA AKIRI CHANGAMOTO YA UHABA WA MADAKTARI

soma pia


WAZIRI WA AFYA AKIRI CHANGAMOTO YA UHABA WA MADAKTARI

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii 

WAZIRI  wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu  amesema kuwa kuna changamoto ya uhaba wa madaktari katika Hospitali ya Rufaa ya Amana jijini Dar es Salaam kutokana na idadi kubwa ya wagonjwa wanaofika kwa ajili ya kupata huduma katika hospitali hiyo.

Ametoa kauli hiyo leo wakati anamalizia ziara yake kwenye hospitali hiyo ambapo amesema pamoja na kuridhishwa na huduma ambazo madaktari wanazitoa kwa wagonjwa katika hospitali hiyo lakini bado kuna changamoto ya uhaba wa madaktari."Nimeridhishwa na huduma katika hospitali hii na nimpongeze Mganga Mfawidhi na uongozi  wa Wilaya  kwa kazi nzuri wanayoifanya licha ya kwamba bado tunafahamu kuna changamaoto katika sekta ya afya.

"Madaktari wa Amana kwa siku wanahudumia wagonjwa 800 , hivyo tunachangamoto ya uhaba wa madaktari na kwa kuwa kuna nafasi za ajira 52,000 zimetangazwa tunaamini sekta ya afya tutapewa mgao unaostaili ili tuwe na wataalamu wa masuala ya afya wa kutosha,"amesema Waziri Mwalimu.Mbali ya changamoto ya uhaba wa madaktari, Waziri Mwalimu ameendelea kuwasisitiza wagonjwa umuhimu wa kuwa na kadi za bima ya afya kwani humfanya anayekuwa nayo kuwa na uhakika wa kupata matibabu kwa gharama nafuu.

"Ifike wakati kila mwananchi awe na kadi ya bima ya afya kwani milango imefunguka na kilichobaki ni kuendelea kuona umuhimu wa kuwa nayo,"amesema Waziri Mwalimu.Wakati huohuo ametoa onyo kwa watumishi wote wa hospitali za Serikali ambao watabainika kujihusisha na tabia ya kuuza dawa ambazo zimetolewa na Bohari ya Dawa(MSD)ambazo zinatolewa bure waache mara moja.
 Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu  akizungumza na wagonjwa waliofika katika Hospitali ya Rufaa ya Amana kwa ajili ya kupatiwa matibabu wakati alipofanya ziara ya kukagua hospitali hizo mara baada ya Rais Dk John Pombe Magufuli kuagiza Hospitali hizo zianze kusimamiwa na Wizara ya Afya.
 Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Amana, Dr Meshack Shimwela  akitoa maelezo kwa Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu  akikagua Dawa zilizopo katika Bohari ya Dawa ya Hospitali ya Rufa aya Amana Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu  akizungumza na Madaktari ndani ya Wodi ya watoto katika Hospitali ya Amana.



Hivyo makala WAZIRI WA AFYA AKIRI CHANGAMOTO YA UHABA WA MADAKTARI

yaani makala yote WAZIRI WA AFYA AKIRI CHANGAMOTO YA UHABA WA MADAKTARI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI WA AFYA AKIRI CHANGAMOTO YA UHABA WA MADAKTARI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/waziri-wa-afya-akiri-changamoto-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAZIRI WA AFYA AKIRI CHANGAMOTO YA UHABA WA MADAKTARI"

Post a Comment