Mkutano wa Kamati ya Ufundi ya Makamishna wa Upelelezi wa Kodi wa Mamlaka za Mapato Afrika Mashariki

Mkutano wa Kamati ya Ufundi ya Makamishna wa Upelelezi wa Kodi wa Mamlaka za Mapato Afrika Mashariki - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mkutano wa Kamati ya Ufundi ya Makamishna wa Upelelezi wa Kodi wa Mamlaka za Mapato Afrika Mashariki, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mkutano wa Kamati ya Ufundi ya Makamishna wa Upelelezi wa Kodi wa Mamlaka za Mapato Afrika Mashariki
kiungo : Mkutano wa Kamati ya Ufundi ya Makamishna wa Upelelezi wa Kodi wa Mamlaka za Mapato Afrika Mashariki

soma pia


Mkutano wa Kamati ya Ufundi ya Makamishna wa Upelelezi wa Kodi wa Mamlaka za Mapato Afrika Mashariki

Na Oliver Njunwa, Zanzibar
Wapelelezi wa Kodi wa Mamlaka za Mapato Afrika Mashariki wametakiwa kuharakisha mchakato wa kuandaa mtaala wa kuwajengea uwezo wapelelezi wa kodi pamoja na mfumo wa kisheria ili kuweza kushirikiana katika kupambana na uhalifu katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Wito huo umetolewa na Kaimu Naibu Kamishna wa Upelelezi wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Salim Kessi wakati akifungua Mkutano wa Wajumbe wa Kamati ya Ufundi ya Makamishna wa Upelelezi wa Kodi wa Mamlaka za Mapato Afrika Mashariki unaofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu Zanzibar.
“Tunataka mchakato huu umalizike mapema ili tuweze kupambana na uhalifu katika ukusanyaji wa kodi kwani kadri tunavyochelewa ndivyo na wahalifu wanaendelea kusababisha upotevu wa kodi kwa mamlaka zetu za mapato”, alisema Bw. Kessi.
Aliongeza kwamba kwa siku nne ambazo watakuwa Zanzibar wanatakiwa kukamilisha hiyo kazi ili iweze kuwasilishwa katika kikao cha Makamishna wa Upelelezi wa Kodi Afrika Mashariki ambao walikubaliana kushirikiana kufanya upelelezi wa kodi kwa pamoja kupampana na kudhibiti uhalifu katika masuala ya kodi.
Aidha aliwapongeza wajumbe wa kamati hiyo ya ufundi kwa jitihada zao ambazo zimewezesha kuundwa kwa chombo cha uendeshaji ambacho kitasaidia ubadilishanaji wa taarifa na upepelelezi wa pamoja katika ukanda wa Afrika Mashariki.
“Ni kutokana na jitihada hizo sasa tayari tuna rasimu ya mkataba wa huduma ambayo itatoa uhalali wa operesheni katika kubadilishana taarifa na upepelezi wa pamoja”, alisisitiza Bw. Kessi na kuongeza kwamba pia kuwepo kwa mwongozo wa upelelezi wa pamoja na kanuni za maadili ni jambo la kujivunia.
Mkutano huo unahudhuriwa na wapelezi wa kodi kutoka Mamlaka za Mapato za Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi na Tanzania ambao ni wajumbe wa Kamati ya Ufundi ya Makamishna wa Upelelezi wa Mamlaka za Mapato Kodi Afrika Mashariki.
Kaimu Naibu Kamishna huyo wa Upelelzi wa Kodi aliwaambia wajumbe hao kwamba ishara ya kwamba mwelekeo wa kushirikiana katika upelelzi ni mzuri inaonekana hata kama chombo cha kisheria hakijakamilika kwani tayari wamebadilishana taarifa za Himaya ya Pamoja ya Forodha na kufanya usuluhishi katika jumuiya.
Naye Meneja wa Upelelezi wa Mamlaka ya Mapato Kenya (KRA) Jonah Ogalo amesema kwamba mkutano huo ni muhimu kwa nchi za Afrika Mashariki katika kuweka mikakati ya pamoja kukabiliana na uhalifu katika ukusanyaji wa kodi na kuongeza kwamba kukamilika kwa mtaala wa mafunzo kwa wapelelezi wa kodi kutawasaidia kushirikiana na kubadilishana taarifa za kiintelijensia na hivyo kuokoa mapato ya serikali.
Kamati ya Ufundi ya wapelelezi wa kodi inatarajiwa kutoa mtaala wa pamoja wa mafunzo ya kuwaongezea ujuzi wapelelezi wa Kodi pamoja na kuunda mfumo wa pamoja wa kisheria utakao wawezesha kufanya upelelezi kwa pamoja kutokana na kila nchi kuwa na sheria zake isipokuwa katika masuala ya Forodha ambapo nchi za Afrika Mashiriki zinatekeleza sheria moja ya Usimamizi wa Forodha.

Kaimu Naibu Kamishna wa Upelelezi wa Kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Salim Kessi akisisitiza jambo wakati akifungua mkutano wa Kamati ya wapelelezi wa Kodi Afrika Mashariki.
Wajumbe wa Kamati ya wapelelezi wa kodi wakifuatilia kwa makini hotuba ya Kaimu Naibu Kamishna wa Upelelezi wa Kodi TRA Salim Kessi (hayupo katika picha) wakati akifungua rasmi mkutano.
Wajumbe wa Mkutano wa Kamati ya Wapelelezi wa Kodi Afrika Mashariki katika picha ya Pamoja na Kaimu Naibu Kamishna wa Upelelezi wa Kodi TRA Salim Kessi (katikati walioketi) mara baada ya ufunguzi wa mkutano katika ukumbi wa Benki Kuu Zanzibar. 


Hivyo makala Mkutano wa Kamati ya Ufundi ya Makamishna wa Upelelezi wa Kodi wa Mamlaka za Mapato Afrika Mashariki

yaani makala yote Mkutano wa Kamati ya Ufundi ya Makamishna wa Upelelezi wa Kodi wa Mamlaka za Mapato Afrika Mashariki Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mkutano wa Kamati ya Ufundi ya Makamishna wa Upelelezi wa Kodi wa Mamlaka za Mapato Afrika Mashariki mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/mkutano-wa-kamati-ya-ufundi-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Mkutano wa Kamati ya Ufundi ya Makamishna wa Upelelezi wa Kodi wa Mamlaka za Mapato Afrika Mashariki"

Post a Comment