title : WAGONJWA 64,093 WATIBIWA KATIKA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE KWA MWAKA 2017
kiungo : WAGONJWA 64,093 WATIBIWA KATIKA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE KWA MWAKA 2017
WAGONJWA 64,093 WATIBIWA KATIKA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE KWA MWAKA 2017
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa mwaka wa 2017 imeona jumla ya wagonjwa 64,093 kati ya hawa wagonjwa wa nje ni 60,796 na waliolazwa 3297. Wagonjwa waliolazwa 3010 waliruhusiwa baada ya hali zao kuwa nzuri na wagonjwa 287 walipoteza maisha hii ikiwa ni sawa na asilimia 8.7.
Wagonjwa 225 walifanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua ambapo wagonjwa 200 waliruhusiwa na wagonjwa 25 walifariki Dunia hii ikiwa ni sawa na asilimia 11 (wastani wa kimataifa ni asilimia 13). Kati ya wagonjwa 225 waliofanyiwa upasuaji wa kufungua kifua wagonjwa 105 walifanyiwa upasuaji na madaktari wetu bingwa wa magonjwa ya moyo watoto wakiwa ni 60 na watu wazima 45.
Upasuaji wa moyo wa bila kufungua kifua (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cathlab ulifanyika kwa wagonjwa 800 kati ya hao 798 wanaendelea vizuri na wagonjwa wawili (2)walifariki hii ikiwa ni chini ya asilimia 1.6. Kati ya wagonjwa 800 waliotibiwa wagonjwa watu wazima 631 walifanyiwa upasuaji na madaktari wetu wa ndani.
Tulikuwa na jumla ya kambi za matibabu 15. Tumefanya matibabu ya pamoja na washirika wetu kutoka mabara ya Asia, Australia, Ulaya na Amerika. Katika kambi zote hizo kambi za watoto ni tano na kambi za watu wazima 10. Jumla ya wagonjwa 120 walifanyiwa upasuaji wa kufungua kifua kati ya hao watoto 80 na watu wazima ni 40. Wagonjwa 169 walifanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua kati ya hao watoto 92 na watu wazima 77.
Kwa wagonjwa wote hao 1025 kufanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na bila kufungua kifua hapa nchini Taasisi imeweza kuokoa zaidi ya bilioni 29 (Tshs. 29,725,000,000/=) ambazo Serikali ingezilipa kama wagonjwa hawa wangefanyiwa upasuaji wa moyo nje ya nchi. Gharama za mgonjwa mmoja anayetibiwa nje ya nchi ugonjwa wa moyo ni zaidi ya milioni 29.
Tulifanya upasuaji wa kuunganisha mishipa ya damu (AVF- Arterio Venous Fistula) kwa ajili ya kusafishia damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo (Hemodialysis) 52.
Hivyo makala WAGONJWA 64,093 WATIBIWA KATIKA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE KWA MWAKA 2017
yaani makala yote WAGONJWA 64,093 WATIBIWA KATIKA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE KWA MWAKA 2017 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAGONJWA 64,093 WATIBIWA KATIKA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE KWA MWAKA 2017 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/wagonjwa-64093-watibiwa-katika-taasisi.html
0 Response to "WAGONJWA 64,093 WATIBIWA KATIKA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE KWA MWAKA 2017"
Post a Comment