title : SIMBA SC WAREJEA DAR KWA RAHA ZAO
kiungo : SIMBA SC WAREJEA DAR KWA RAHA ZAO
SIMBA SC WAREJEA DAR KWA RAHA ZAO
Na Agness Francis, Globu ya Jamii.
KIKOSI cha Wekundu wa Msimbazi Simba SC kimewasili leo jijini Dar es Salaam kikitokea mkoani Kagera kilikokuwa na mchezo wake dhidi ya Kagera Sugar.
Mchezo huo uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Kaitaba ambapo Simba wameibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Akizungumza na Michuzi Blog baada ya kuwasili leo,jijini Dar es Salaam katika uwanja kimataifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Kocha Msaidizi wa Simba Massoud Djuma amesema kuwa anawashukuru wachezaji wake kwa kufanya vizuri kwenye Ligi kuu Tanzania Bara.
Amesema anaamini watafika mbali wakiendelea kucheza kwa kumsikiliza Mwalimu. Aidha Mwalimu huyo amewapongeza wachezaji kwa jinsi wanavyojituma." Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mungu tumerejea salama, pia niwapongeze wachezaji wangu kwa kuendelea kufanya vizuri kwenye Ligi Kuu, naimani tukicheza kwa ushirikiano tutazidi kufanya vizuri zaidi na zaidi,"amesema Masoud
Wakati huohuo mchezaji Shomari Kapombe baada ya takribani miezi sita aliyokuwa akiumwa jana amepata nafasi ya kucheza na ameonesha kiwango kikubwa katika mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar na kutengeneza nafasi ya goli la pili ililofungwa na John Bocco dakika ya 79.
Kapombe amesema kuwa anamshuru mwalimu (Massoud Djuma) kwa kumuamini na kumpa nafasi ya kucheza mchezo wa jana na anaamini ataendelea kufanya vizuri katika Kikosi cha Wekundu wa Msimbazi.
Mchezaji wa wekundu wa Msimbazi SimbaSc Shomari Kapombe akizungumza na waandishi wa habari alipowasili leo Jijini Dar Es Salaam katika uwanja wa Mwalimu J.K. Nyerere.
Kocha Msaidizi wa Simba Massoud Djuma akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwa sili leo Jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa kimataifa Mwalimu J.K. Nyerere akiwapongeza wachezaji ea Kikosi hicho kwa kufata maelekezo yake na kufanya vizuri.
Hivyo makala SIMBA SC WAREJEA DAR KWA RAHA ZAO
yaani makala yote SIMBA SC WAREJEA DAR KWA RAHA ZAO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SIMBA SC WAREJEA DAR KWA RAHA ZAO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/simba-sc-warejea-dar-kwa-raha-zao.html
0 Response to "SIMBA SC WAREJEA DAR KWA RAHA ZAO"
Post a Comment