SERIKALI YAMKABA SHINGO DANGOTE

SERIKALI YAMKABA SHINGO DANGOTE - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI YAMKABA SHINGO DANGOTE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI YAMKABA SHINGO DANGOTE
kiungo : SERIKALI YAMKABA SHINGO DANGOTE

soma pia


SERIKALI YAMKABA SHINGO DANGOTE

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ametoa siku 14 kwa uongozi wa kiwanda cha saruji cha Dangote mkoa wa Mtwara kuingia mkataba na wachimbaji wadogo wa gypsum.
Biteko ametoa kauli hiyo leo Januari 21, 2018 baada ya kutembelea kiwanda hicho na kuzungumza na viongozi wake.
Amesema mikataba hiyo inapaswa kuwa na kipengele cha kuwalipa ndani ya siku 30 baada ya kiwanda kukusanya gypsum kutoka kwa wachimbaji hao, lengo likiwa ni kuleta ufanisi na tija katika biashara zao.
“Nimekubaliana hapa kamishna wa kanda atasimamia hili la mikataba kati ya kiwanda na wachimbaji wa gypsum. Sehemu ya malipo itakuwa ndani ya mkataba na watalipa ndani ya siku 30,” amesema.
Amesema wachimbaji hao wamekuwa wakilalamikia kucheleweshewa malipo yao baada ya kupeleka kiwandani bidhaa zao.
“Nimeambiwa wachimbaji hawa walikuwa wanalipwa baada ya miezi mitatu lakini kwa mkataba huu ambao wataingia na kiwanda sasa watakuwa wanalipwa ndani ya siku 30,” amesema Biteko.
Amesema Serikali ya Awamu ya Tano inalenga kuwasaidia wachimbaji wadogo sambamba na wawekezaji ambao wanapaswa kufanya kazi bila kusumbuliwa.
“Uwepo wa kiwanda hiki unawasaidia wachimbaji wetu waweze kupata bei nzuri pamoja na kupata soko la uhakika la kuuza bidhaa zao. Dangonte wameniahidi kwamba ndani ya muda mfupi watatekeleza agizo hili,” amesema.
Biteko amesema lengo la ziara yake ni kuwasaidia wachimbaji wa gypsum ambao hawana mikataba na kujikuta wakibanwa katika uuzaji wa bidhaa zao.
Chanzo- Mwananchi


Hivyo makala SERIKALI YAMKABA SHINGO DANGOTE

yaani makala yote SERIKALI YAMKABA SHINGO DANGOTE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YAMKABA SHINGO DANGOTE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/serikali-yamkaba-shingo-dangote.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SERIKALI YAMKABA SHINGO DANGOTE"

Post a Comment