Reli ya ‘Standard Gauge” Sasa Dar Mpaka Rwanda

Reli ya ‘Standard Gauge” Sasa Dar Mpaka Rwanda - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Reli ya ‘Standard Gauge” Sasa Dar Mpaka Rwanda, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Reli ya ‘Standard Gauge” Sasa Dar Mpaka Rwanda
kiungo : Reli ya ‘Standard Gauge” Sasa Dar Mpaka Rwanda

soma pia


Reli ya ‘Standard Gauge” Sasa Dar Mpaka Rwanda

Na. Judith Mhina 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa Tanzania na Rwanda zimekubaliana kuunganisha Reli ya Kisasa (Standard Gauge) kutoka Isaka mkoani Shinyanga mpaka Kigali nchini Rwanda, ili kukuza biashara na uchumi wa nchi hizi mbili.

Rais Magufuli ameeleza hayo leo Ikulu Jijini Daar es Salaam muda mfupi baada ya kufanya mazungumzo na Rais wa Rwanda, Mhe. Paul Kagame aliyekuja nchini kwa ziara ya kikazi ya siku moja.“Mimi na Rais Kagame kumeongea mambo mengi ya ushirikiano na kwa pamoja tumekubaliana kuanza ujenzi wa Reli ya Standard Gauge kutoka Isaka mpaka Kigali,” ameeleza Rais Magufuli.

Ameeleza kuwa ili kuharakisha ujenzi wa reli hiyo, kwa pamoja wamewaagiza Mawaziri wanaohusika na sekta ya ujenzi na wale wale wa Mambo ya Nje wa nchi hizi mbili kukutana haraka wiki ijayo kusughulikia masuala kadhaa yanayohusu ujenzi wa reli hiyo ikiwa ni pamoja na kujadili namna ya upatikanaji wa fedha za ujenzi.

Akielezea umuhimu wa kukuza uchumi na biashara baina nchi hizi mbili, Rais Magufuli amesema mpaka sasa mwenendo wa biashara kati ya nchi hizi umekuwa wa kusuasua na kwamba reli hiyo itasaidia kuimarisha biashara na ushirikiano wa Tanzania na Rwanda.

“Tunataka ikifika mwezi Desemba mwaka huu, mimi na Rais Kagame tuwe tayari tumeweka mawe ya msingi kwa ajili ya kuanza ujenzi wa reli hii,” alisisitiza Rais Magufuli.

Amesisitiza kuwa mbali na kuimarisha uchumi, ujenzi wa reli hiyo yenye urefu wa takribani kilometa 400 pia utatoa ajira kwa vijana wengi na kusaidia usafirishaji wa madini ya Nickel kutoka nchi za Rwanda, Burundi na Tanzania ambapo madini hayo yanashindwa kuchimbwa kutokana na kukosekana usafiri madhubuti wa reli.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amesema kwamba Tanzania inamuunga mkono Rais Kagame kwa asilimia mia moja katika kuchukua Uenyekiti wa Umoja wa Afrika na kwamba itafanya kila linalowezekana kuzishawishi nchi marafiki pia zimuunge mkono Rais huyo wa Rwanda.

Kwa upande wake, Rais Paul Kagame amemshukuru Rais Magufuli na Watanzania kwa kumuunga mkono katika nafasi ya Uenyekiti wa Umoja wa Afrika na kwamba atafanya kila linalowezekana kuzishawishi nchi za Afrika kuongeza uwekezaji na kila nchi kuweka kikakati ya kuongeza ajira ili kuwafanya vijana waachane na dhana ya kukimbili nchi za Ulaya kutafuta maisha bora.



Hivyo makala Reli ya ‘Standard Gauge” Sasa Dar Mpaka Rwanda

yaani makala yote Reli ya ‘Standard Gauge” Sasa Dar Mpaka Rwanda Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Reli ya ‘Standard Gauge” Sasa Dar Mpaka Rwanda mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/reli-ya-standard-gauge-sasa-dar-mpaka.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Reli ya ‘Standard Gauge” Sasa Dar Mpaka Rwanda"

Post a Comment