title : MPINA ATEKETEZA ZANA HARAMU ZA UVUVI ZENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 2 WILAYANI UKEREWE
kiungo : MPINA ATEKETEZA ZANA HARAMU ZA UVUVI ZENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 2 WILAYANI UKEREWE
MPINA ATEKETEZA ZANA HARAMU ZA UVUVI ZENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 2 WILAYANI UKEREWE
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Mhe Luhaga Mpina ametaifisha na kuteketeza zana haramu za uvuvi zenye thamani ya shilingi bilioni 2 zilizokamatwa wakati zikitumika kwa shughuli za uvuvi katika visiwa vidogo vilivyopo ndani ya Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza huku Shilingi milioni 120 zikikusanywa kama sehemu ya adhabu kwa wavuvi na wafanyabiashara waliokutwa na zana haramu pamoja na makosa ya utoroshaji samaki na mazao yake nje ya nchi.
Waziri Mpina aliwaonya watu wanaotumia majina ya wavuvi kutishia kufanya migomo isiyoisha na kuandamana baada ya uamuzi wa Serikali kuanza kuchukua hatua stahiki za kudhibiti uvuvi haramu, na kwamba msimamo uliowekwa na Serikali ni thabiti na usiyoyumba hivyo migomo na maandamano ya watu wenye lengo la kukwamisha vita dhidi ya uvuvi haramu haitasaidia chochote na badala yake operesheni kali isiyo na mwisho itaendelea hadi pale uvuvi haramu utakapokoma ndani ya Ziwa Victoria.
“Rasilimali zilizopo ndani ya ziwa hili ni mali ya wananchi sisi viongozi mliotupa dhamana ya kuongoza kazi yetu ni ulinzi tu na endapo tutakomesha uvuvi haramu nyie ndio mtakaonufaika hivyo ni itashangaza tajiri aliyempa kibarua cha ulinzi, na mlinzi huyo akafanya kazi vizuri ya kulinda mali za bosi wake alafu tajiri akamlalamikia kibarua wake sisi na watendaji wa Serikali ni vibarua tu wenye mali ni ninyi hatua tunazochukua zitaleta manufaa makubwa kwenu”alisema.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina (mwenye miwani) baada ya kuwasili kwenye kambi ya Uvuvi ya Kisiwa cha Galinzila leo na kuongea na wavuvi. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Estomiah Chang’a (mwenye kofia) na kulia zaidi ni Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Ukerewe Frank Bahati leo. Mhe. Mpina alichoma moto nyavu haramu za uvuvi zenye thamani ya shilingi bilioni mbili. (Na John Mapepele)
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina (mwenye miwani) akiwahutubia wavuvi kwenye kambi ya wavuvi katika kisiwa cha Galinzila Wilayani Ukerewe ambapo baadaye alichoma moto nyavu haramu za uvuvi zenye thamani ya shilingi bilioni mbili katika kijiji Kakukuru.
Umati wa wavuvi kwenye kambi ya wavuvi ya Kisiwa cha Galinzila wilayani Ukerewe wakimsikiliza Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina (hayupo pichani) ambapo baadaye alichoma moto nyavu haramu za uvuvi zenye thamani ya shilingi bilioni mbili katika kijiji cha Kakukuru zilizokamatwa katika operesheni maalum ya siku tano ya kutokomeza uvuvi haramu katika Wilaya ya Ukerewe leo.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akiwa katika picha ya pamoja na kikosi kazi kilichofanya operesheni ya kutokomeza uvuvi haramu katika Wilaya ya Magu na Busega mara baada ya kuteketeza kwa kuchoma moto zana haramu za uvuvi zenye thamani ya Tsh 457,075,000/= katika kijiji cha Kageye wilayani Magu leo.
Hivyo makala MPINA ATEKETEZA ZANA HARAMU ZA UVUVI ZENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 2 WILAYANI UKEREWE
yaani makala yote MPINA ATEKETEZA ZANA HARAMU ZA UVUVI ZENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 2 WILAYANI UKEREWE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MPINA ATEKETEZA ZANA HARAMU ZA UVUVI ZENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 2 WILAYANI UKEREWE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/mpina-ateketeza-zana-haramu-za-uvuvi.html
0 Response to "MPINA ATEKETEZA ZANA HARAMU ZA UVUVI ZENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 2 WILAYANI UKEREWE"
Post a Comment