title : JK AFURAHIA SOMO LA MKIKITA KUHUSU KILIMO BORA CHA PAPAI
kiungo : JK AFURAHIA SOMO LA MKIKITA KUHUSU KILIMO BORA CHA PAPAI
JK AFURAHIA SOMO LA MKIKITA KUHUSU KILIMO BORA CHA PAPAI
Na Richard Mwaikenda, Msoga.
.RAIS mstaafu Dk.Jakaya Kikwete amefurahishwa na elimu ya kilimo cha kisasa cha Papai chenye gharama nafuu aliyopatiwa na Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita/Living green)
Elimu hiyo ilitolewa hivi karibuni nyumbani kwake Msoga, Chalinze, mkoani Pwani na Ezra Machogu Mtaalamu wa Kilimo wa Kampuni ya Awino Farm ambayo ni mwanachama wa Mkikita.
Kikwete alifurahi kuambiwa kwamba kampuni hiyo inaweza kuzalisha papai lenye ubora kwa kutumia teknolojia ya kisasa yenye gharama nafuu hivyo kumfanya mkulima apate faida kubwa wakati wa mauzo.
Ezra anasema kuwa unaweza kupunguza gharama kwa kuacha kuchimba mashimo badala yake unalima shamba mara tatu kwa kutumia trekta, hivyo kuufanya udongo kuwa tifutifu kitendo kitakacho kurahisishia kupanda miche ya papai bila matatizo.
Anasema ukitumia njia hiyo itakuondolea gharama ya kuchimba mashimo 1200 katika heka moja ambayo jumla ni sh. mil. 6 ikiwa kila shimo itakuwa sh. 500 wakati kulima mara tatu heka moja kwa trekta ni sh. 150,000.
Ezra anamweleza Dk. Kikwete kuwa unaweza pia kupunguza gharama ya mbolea kwa kila shimo kuweka majagi mawili badala ya debe moja.Pia alimweleza kuwa katika umwagiliaji papai halihitaji maji mengi, hivyo unaweza kutumia lita 10,000 kwa siku kumi badala ya siku nne.
Meneja Kilimo wa Mashamba ya Dk. Kikwete, Justine (kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Awino, Martine Wamaya (kulia) na Mtalaamu wa kilimo cha Papai, Ezra Machogu walipokuwa wakitoka kuchuma papai kutoka kwenye shamba darasa la Kampuni ya Awino eneo la Msata tayari kumpelekea Rais mstaafu, Dk. Kikwete.
Hivyo makala JK AFURAHIA SOMO LA MKIKITA KUHUSU KILIMO BORA CHA PAPAI
yaani makala yote JK AFURAHIA SOMO LA MKIKITA KUHUSU KILIMO BORA CHA PAPAI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala JK AFURAHIA SOMO LA MKIKITA KUHUSU KILIMO BORA CHA PAPAI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/jk-afurahia-somo-la-mkikita-kuhusu.html
0 Response to "JK AFURAHIA SOMO LA MKIKITA KUHUSU KILIMO BORA CHA PAPAI"
Post a Comment