IKULU YATOA TAARIFA HII BAADA YA FAMILIA YA BABU SEYA KUZULU IKULU LEO.

IKULU YATOA TAARIFA HII BAADA YA FAMILIA YA BABU SEYA KUZULU IKULU LEO. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa IKULU YATOA TAARIFA HII BAADA YA FAMILIA YA BABU SEYA KUZULU IKULU LEO., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : IKULU YATOA TAARIFA HII BAADA YA FAMILIA YA BABU SEYA KUZULU IKULU LEO.
kiungo : IKULU YATOA TAARIFA HII BAADA YA FAMILIA YA BABU SEYA KUZULU IKULU LEO.

soma pia


IKULU YATOA TAARIFA HII BAADA YA FAMILIA YA BABU SEYA KUZULU IKULU LEO.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 02 Januari 2018 amekutana na Mwanamuziki Nguza Viking na watoto wake waliofika Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kumshukuru kwa kupatiwa msamaha wa kuachiwa huru kwake Nguza Viking (Babu Seya) na Mwanae Papii Nguza (Papii Kocha) waliokuwa wakitumia adhabu ya kifungo cha maisha jela.

Nguza Viking na Papii Nguza wakiwa na wana familia wengine Nguza Mbangu na Francis Nguza wamezungumza na Mhe. Rais Magufuli ambapo wamemshukuru kwa msamaha alioutoa kwao na kwa wafungwa wengine 61 waliokuwa wamehukumiwa adhabu ya kifo, na wamemuahidi kuwa raia wema na watachapa kazi kwa juhudi na maarifa.

“Yaani sijui nisemaje, hapa nina furaha kubwa sana moyoni mwangu, nilikuwa naomba sana tangu muda mrefu nikutane nae, nimeomba sana sana, hatimaye leo nimefanikiwa na nimemwambia namshukuru sana kwa kutusamehe na sasa nipo tayari kuchapa kazi, Hapa Kazi Tu” amesema Nguza Viking na kuungwa mkono na mwanae Papii Nguza.

Nguza Viking na wanae wamemuombea Mhe. Rais Magufuli na wameiombea nchi, na pia msemaji wa familia hii Nguza Mbangu amesema wanajipanga kuendeleza kazi zao za sanaa.

Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli amewashukuru kwa kuja kumuona na kumshukuru lakini amesema shukrani zimwendee Mwenyezi Mungu ambaye ndiye husamehe.

“Najua mmekuwa mkihangaika kutaka kuniona, nikaona wacha niwasikilize, hata hivyo mshukuruni Mwenyezi Mungu ambaye ndiye hutoa msamaha, sasa nendeni mkachape kazi, na mmtangulize Mungu” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli ametia saini kitabu cha maombolezo na kumpa pole Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Kangi Alphaxard Lugola aliyefiwa na Mkewe Kamishna Msaidizi wa Polisi Mary Lugola.

Kamishna Msaidizi wa Polisi Mary Lugola amefariki dunia jana asubuhi tarehe 01 Januari, 2018 katika hospitali ya Rabinisia iliyopo Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu na msiba upo Gerezani Railway Club Jijini Dar es Salaam.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasilino ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
02 Januari, 2018


Hivyo makala IKULU YATOA TAARIFA HII BAADA YA FAMILIA YA BABU SEYA KUZULU IKULU LEO.

yaani makala yote IKULU YATOA TAARIFA HII BAADA YA FAMILIA YA BABU SEYA KUZULU IKULU LEO. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala IKULU YATOA TAARIFA HII BAADA YA FAMILIA YA BABU SEYA KUZULU IKULU LEO. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/ikulu-yatoa-taarifa-hii-baada-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "IKULU YATOA TAARIFA HII BAADA YA FAMILIA YA BABU SEYA KUZULU IKULU LEO."

Post a Comment