title : HESLB kuanza kuwasaka wadaiwa sugu 119,497 jumatatu ijayo
kiungo : HESLB kuanza kuwasaka wadaiwa sugu 119,497 jumatatu ijayo
HESLB kuanza kuwasaka wadaiwa sugu 119,497 jumatatu ijayo
* Wanadaiwa Tshs 285 bilioni
* Ukaguzi kwa waajiri pia kufanyika
Na Mwandishi Wetu
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) wiki ijayo (Jumatatu, Januari 8, 2018) inatarajia kuanza kuwasaka jumla ya wanufaika 119,497 nchini kote ambao wamekiuka sheria iliyoanzisha Bodi hiyo kwa kutoanza kurejesha mikopo yenye thamani ya TZS 285 bilioni waliyokopeshwa tangu mwaka 1994/1995 na mikopo yao imeiva lakini hawajaanza kurejesha.
Aidha, Bodi ya Mikopo inatarajia kuanza kufanya ukaguzi kwa waajiri mbalimbali nchini kote ili kubaini kama katika orodha za waajiriwa wao (payrolls) kuna wanufaika wa mikopo ambao hawajaanza kurejesha.
Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru (pichani) amesema leo (Jumatano, Januari 3, 2018) jijini Dar es Salaam kuwa msako huo utafanywa kwa miezi mitatu kuanzia wiki ijayo (Jumatatu, Januari 8, 2018).
Bw. Badru ametoa kauli hiyo wakati akitoa tathmini ya utekelezaji wa majukumu ya Bodi ya Mikopo kwa nusu ya mwaka wa fedha wa 2017/2018 uliomalizika Desemba 31, 2017. Katika tathmini hiyo, Bw. Badru alizungumzia mafanikio, changamoto na mipango ya kuboresha ufanisi katika utoaji wa mikopo ya elimu ya juu na ukusanyaji wa mikopo iliyoiva.
Maafisa wa Bodi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Serikali wamejipanga katika kutekeleza hili ili kuongeza makusanyo ya mwezi kutoka wastani wa TZS 13 bilioni hivi sasa hadi kufikia TZS 17 bilioni mwezi Juni, 2018.
Orodha kamili ya waajiri na wanufaika wa mikopo ambao wanakiuka Sheria ya Bodi ya Mikopo (SURA 178) kwa kutowasilisha makato au kurejesha mikopo ya elimu ya juu inapatikana katika tovuti ya Bodi ya Mikopo (www.heslb.go.tz) kuanzia leo (Jumatano, Januari 3, 2018).
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Abdul-Razaq Badru akiongea na wanahabari leo (Jumatano, Jan. 3, 2018) jijini Dar es Salaam ambapo alielezea utekelezaji wa majukumu ya taasisi yake katika nusu ya mwaka 2017/2018 na kuanza kwa kampeni ya kuwasaka wanufaika sugu wa mikopo 119,497 ambao hawajaanza kurejesha. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Upangaji Mikopo Dkt. Veronika Nyahende na kushoto ni PHIDELIS Joseph, Mkurugenzi Msaidizi wa Urejeshaji Mikopo (Picha na Happiness Kihwele- HESLB).
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala HESLB kuanza kuwasaka wadaiwa sugu 119,497 jumatatu ijayo
yaani makala yote HESLB kuanza kuwasaka wadaiwa sugu 119,497 jumatatu ijayo Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HESLB kuanza kuwasaka wadaiwa sugu 119,497 jumatatu ijayo mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/heslb-kuanza-kuwasaka-wadaiwa-sugu.html
0 Response to "HESLB kuanza kuwasaka wadaiwa sugu 119,497 jumatatu ijayo"
Post a Comment