title : Helioum One yagundua heliamu ya futi za ujazo bilioni 98.9
kiungo : Helioum One yagundua heliamu ya futi za ujazo bilioni 98.9
Helioum One yagundua heliamu ya futi za ujazo bilioni 98.9
Kampuni ya uchunguzi na utafiti wa madini, Helium One, ambayo kwa sasa inafanya utafiti wa gesi ya heliamu mkoa wa Rukwa imegundua kuwapo kwa futi za ujazo bilioni 98.9 za gesi hiyo katika maeneo iliyokwishafanyia uchunguzi. Hayo yalielezwa katika warsha ya siku moja iliyofanyika Chuo Kikuu cha Dar es salaam, na kuratibiwa na Idara ya Jiolojia ya chuo hicho, Helium One na Chuo Kikuu cha Oxford.
Akizungumza katika warsha hiyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Helium One, Thomas Abraham-James, alisema kwamba kampuni yao imetafuta leseni 23 za uchunguzi na kwamba nyingine tatu zimeombwa.Alisema kwamba leseni hizo zote zinamilikiwa na kampuni hiyo kwa asilimia 100 na kwamba ina haki za kipekee za gesi hiyo ya heliamu .
Pamoja na kutoa taarifa hiyo,alisema lengo la kuwa na warsha ni kuwaita wataalamu na wadau mbalimbali wa hapa nchini na kimataifa ubadilishana uzoefu na taarifa zilizopo kuhusu gesi hiyo na kuangalia fursa zinazoambatana na uwapo wa gesi hiyo katika harakati za kitaifa za kuwa na taifa la viwanda.
“Helium One inaamini kwamba kuna fursa kupitia utafiti huu kuweza kutengeneza utaalamu wa kiwango cha juu na utaalamu wa hapa nchini juu ya uendelezaji wa gesi hiyo. Tutaendelea kujenga uhusiano na Chuo Kikuu cha Dar es salaam kuweza kubadilishana elimu, kutoa mafunzo kwa wanafunzi na maofisa wizara ya madini na kutengeneza mpango wa ufadhili wa masomo,” alisema.
Hivyo makala Helioum One yagundua heliamu ya futi za ujazo bilioni 98.9
yaani makala yote Helioum One yagundua heliamu ya futi za ujazo bilioni 98.9 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Helioum One yagundua heliamu ya futi za ujazo bilioni 98.9 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/helioum-one-yagundua-heliamu-ya-futi-za.html
0 Response to "Helioum One yagundua heliamu ya futi za ujazo bilioni 98.9"
Post a Comment