title : Donald Trump atuma salamu kwa viongozi wa Afrika
kiungo : Donald Trump atuma salamu kwa viongozi wa Afrika
Donald Trump atuma salamu kwa viongozi wa Afrika
Rais wa Marekani Donald Trump amemuomba Rais wa Rwanda Paul Kagame ambaye kwa sasa ndiye mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) kufikisha salamu zake kwa viongozi wengine wa mataifa wanachama wa AU.
Viongozi hao wawili wamekutana mjini Davos, Uswizi pambizoni mwa mkutano wa viongozi na watu mashuhuri kuhusu uchumi na biashara duniani.
Mkutano huo wa Kagame na Trump umetokea wiki chache baada ya kiongozi huyo wa Marekani kuyaeleza mataifa ya Afrika kama "machafu" au mataifa ya "mabwege".
Hatua hiyo ilimfanya kushutumiwa vikali na viongozi wa AU na baadhi ya viongozi wa nchi za Afrika kama vile Botswana na Ghana.Bw Trump amekanusha kwamba alitumia neno hilo kuyaelezea mataifa ya Afrika.
Hata hivyo alikiri kwamba alitumia maneno makali akiyaeleza mataifa ya Afrika, Haiti na El Salvador alipokuwa anazungumzia wahamiaji wanaoingia Marekani.
Lakini katika mkutano wake na Kagame pambizoni mwa Mkutano wa Uchumi wa Dunia mjini Davos, Trump hajaonyesha dalili zozote za majuto kuhusu tamko lake la awali kuhusu Afrika.
Hivyo makala Donald Trump atuma salamu kwa viongozi wa Afrika
yaani makala yote Donald Trump atuma salamu kwa viongozi wa Afrika Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Donald Trump atuma salamu kwa viongozi wa Afrika mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/donald-trump-atuma-salamu-kwa-viongozi.html
0 Response to "Donald Trump atuma salamu kwa viongozi wa Afrika"
Post a Comment