title : Dkt. Abbas Ahamasisha Wanahabari Kushiriki Tuzo za SADC
kiungo : Dkt. Abbas Ahamasisha Wanahabari Kushiriki Tuzo za SADC
Dkt. Abbas Ahamasisha Wanahabari Kushiriki Tuzo za SADC
Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas amewahamasisha Waandishi wa Habari wa Tanzania kushiriki vema katika kuwania tuzo za wanahabari wa Jumuiya za Mendeleo Kusini mwa Bara la Africa (SADC).
Dkt. Abbas ametoa rai kwa Waandishi wa Habari kushiriki tuzo hizo jumatatu wiki hii wakati akiongea na waandishi wa Habari kuhusu hali ya uchumi na utekelezaji wa miradi mbalimbali iliyopo nchini. “Tunawaomba wale wote ambao wanadhani wanavigezo basi washiriki tuzo hizi za umahiri ambazo zinahusu waandishi wa habari za magazeti, redio, televisheni na wapiga picha za habari”, alieleza Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali.
Alieleza kuwa maelezo kamili juu ya tuzo hizo yanapatikana katika tovuti ya Idara ya Habari ya www.maelezo.go.tz hivyo wote wenye habari mahiri katika magazeti, vipindi vizuri vya luninga au wapiga picha wahakikishe wanashiriki ili kushindana na waandishi wenzao kutoka nchi za kusini mwa Afrika.
Mbali na tuzo za SADC, Dkt. Abbas pia ameeleza kuwa tuzo nyingine ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) inashindaniwa na Wanahabari na maelezo yake yanapatikana katika tovuti ya Idara ya Habari.
Amewataka wanahabari kuandika habari zao kwa umahiri mkubwa ambazo kwa namna moja ama nyingine zinaweza kukidhi hata kupata tuzo za waandishi bora kama hizo zilizojitokeza. Pamoja na kuwataka waandishi wa habari kushiriki katika tuzo hizo, pia amewataka waandihsi hao kuhakikisha wanapata vitambulisho vipya ya Waandishi wa Habari (Press Cards) vya mwaka 2018 baada ya vile vya mwaka jana kuisha muda wake.
“Kwa kweli mwaka huu tutakuwa wakali kidogo kwa wale ambao hawatokuwa na vitambulisho hivi kwani mchakato wa kuvipata ni rahisi kwa sababu tumeshawapa muda wa miaka mitano wa kwenda kusoma hivyo hatuhitaji vyeti, kinachohitajika ni barua ya mwajiri au chombo cha habari unachofanyia kazi tu.” Alisema Dkt. Abbas.
Aidha, Dkt. Abbas amewakumbusha wanahabari ambao bado kiwango chao cha elimu kipo chini ya kile kilichowekwa katika Sheria ya Huduma za Habari namba 12 ya mwaka 2016 na Kanuni zake za mwaka 2017 kujiendeleza kwani muda uliotolewa wa miaka mitano unaendelea unazidi kuisha.
Hivyo makala Dkt. Abbas Ahamasisha Wanahabari Kushiriki Tuzo za SADC
yaani makala yote Dkt. Abbas Ahamasisha Wanahabari Kushiriki Tuzo za SADC Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Dkt. Abbas Ahamasisha Wanahabari Kushiriki Tuzo za SADC mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/dkt-abbas-ahamasisha-wanahabari.html
0 Response to "Dkt. Abbas Ahamasisha Wanahabari Kushiriki Tuzo za SADC"
Post a Comment