PROF. MAGHEMBE AFUNGUA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTALII DUNIANI MKOANI IRINGA

PROF. MAGHEMBE AFUNGUA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTALII DUNIANI MKOANI IRINGA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa PROF. MAGHEMBE AFUNGUA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTALII DUNIANI MKOANI IRINGA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : PROF. MAGHEMBE AFUNGUA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTALII DUNIANI MKOANI IRINGA
kiungo : PROF. MAGHEMBE AFUNGUA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTALII DUNIANI MKOANI IRINGA

soma pia


PROF. MAGHEMBE AFUNGUA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTALII DUNIANI MKOANI IRINGA

Na Hamza Temba-WMU

Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe jana tarehe 30 Septemba, 2017 amefungua rasmi Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani yanayofanyika kitaifa mkoani Iringa na kutoa wito kwa wananchi kushirikiana na Serikali katika kupambana na Ujangili kwa kutoa taarifa za siri zitakazoweza kuwaibaini na kuchukuliwa hatua.

“Ili kulinda uwepo wa rasilimali za utalii zilizopo kwa vizazi vya sasa na vijavyo, ni lazima wananchi kushirikiana pamoja na Serikali katika mapambano dhidi ya ujangili, mkiona mtu ananyemeleanyemelea huko porini tuambieni tutamshukia kama mwewe” alisisitiza Prof. Maghembe.

Ufunguzi huo wa Siku ya Utalii Kitaifa umeenda sambamba na ufunguzi wa Maonesho ya Karibu Kusini pamoja na maonesho ya wajasiariamali wa viwanda vidogo SIDO yaliyoshirikisha wajasirimali kutoka mikoa ya nyanda zajuu kusini kwa lengo la kuonesha bidhaa zao zitakazoweza kutumiwa na watalii pamoja na watoa huduma hiyo. 

Alisema, kaulimbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu kwa upande wa Siku ya Utalii Duniani ni “Utalii Endelevu” – Ni chombo cha maendeleo wakati ile ya Maonesho ya Karibu Kusini ikiwa ni “Utalii endelevu ni nguzo ya Uchumi wa Viwanda”.

Alisema sekta ya utalii imechangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi kwa kuchangia asilimia kubwa ya mapato ya Serikali, kuongeza ajira, kipato cha jamii na kuchochea ukuaji wa sekta zingine. 

"Utalii ndio ndio sekta pekee inayoongoza kwa kuliingizia taifa fedha za kigeni kwa asilimia 25, Aidha, inachangia asilimia 17.5 ya pato la taifa na asilimia 11 ya ajira zote nchini" alisema prof. Maghembe. 
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Mkakati wa Utalii wa Mkoa wa Iringa ambao umeandaliwa kwa lengo kuunga mkono azma ya Serikali wa kufungua utalii wa Nyanda za Juu Kusini katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana. Kulia ni Mkuu wa Mkoa huo, Amina Masenza na Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Asia Abdallah. Kauli Mbiu za maadhimisho hayo yatakayofikia tamati tarehe 2 Oktoba ni “Utalii Endelevu” – Ni chombo cha maendeleo na “Utalii endelevu ni nguzo ya Uchumi wa Viwanda”. 
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto), Naibu Waziri, Mhandisi Ramo Makani (kulia), Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza (wa tatu kushoto) na viongozi wengine wa Serikali wakionesha Mkakati wa Utalii na Jarida la Iringa baada ya uzinduzi rasmi.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii, Philip Chitaunga akiwa na baadhi ya washiriki wengine kwenye ufunguzi wa maadhimisho hayo.
Sehemu ya washiriki wa maadhimisho hayo ya Wiki ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini. Nyuma yao ni mabanda ya maonesho hayo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala PROF. MAGHEMBE AFUNGUA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTALII DUNIANI MKOANI IRINGA

yaani makala yote PROF. MAGHEMBE AFUNGUA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTALII DUNIANI MKOANI IRINGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala PROF. MAGHEMBE AFUNGUA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTALII DUNIANI MKOANI IRINGA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/prof-maghembe-afungua-maadhimisho-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "PROF. MAGHEMBE AFUNGUA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTALII DUNIANI MKOANI IRINGA"

Post a Comment