title : MKAZI WA TABORA MATATANI KWA KUMILIKI KIWANDA CHA BUNDUKI.
kiungo : MKAZI WA TABORA MATATANI KWA KUMILIKI KIWANDA CHA BUNDUKI.
MKAZI WA TABORA MATATANI KWA KUMILIKI KIWANDA CHA BUNDUKI.
Jeshi la Polisi Mkoani Tabora linamshikilia Mrisho Juma Mlela (44) mnyamwezi, kwa tuhuma za kumiliki kiwanda cha kutengeneza silaha za moto (bunduki).
Akizungumzana na waandishi wa habari, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani hapa ACP Emanuel Nley alisema mtuhumiwa huyo ni mkulima mkazi wa kitongoji cha Songambele kijiji cha Kinamagi kata ya Kigwa wilaya ya Uyui mkoani Tabora.
Amesema mtuhumiwa alikamatwa mnamo Septemba 2 mwaka huu majira ya saa 11.15 jioni baada ya kikosi kazi cha Jeshi hilo kupata taarifa za siri kutoka kwa wananchi wema ambazo zilisaidia kunaswa kwake.
Amesema baada ya kukamatwa na kuhojiwa kwa kina na Jeshi la Polisi mtuhumiwa alikiri kumiliki kiwanda hicho cha kutengeneza silaha za aina mbalimbali.
‘Baada ya kumfanyia upekuzi tumemkuta akiwa na silaha tatu aina ya gobore na pistol moja na vyote vimetengenezwa kienyeji katika kiwanda chake hicho’, amesema Nley.
Aidha kamanda Nley ameongeza kuwa mtuhumiwa huyo amekiri kuwa yeye ndiye katengeneza silaha hizo na alikuwa akiwauzia watu katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.
Kamanda Nley alitoa wito kwa wananchi wote wa mkoa huo wanaomiliki silaha za moto kinyume na taratibu kuzisalimisha haraka katika kituo chochote cha polisi, kwani msako unaoendelea katika mkoa huo hautamwacha salama mtu yeyote anayemiliki silaha ya moto kinyume na utaratibu.
Hivyo makala MKAZI WA TABORA MATATANI KWA KUMILIKI KIWANDA CHA BUNDUKI.
yaani makala yote MKAZI WA TABORA MATATANI KWA KUMILIKI KIWANDA CHA BUNDUKI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MKAZI WA TABORA MATATANI KWA KUMILIKI KIWANDA CHA BUNDUKI. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/mkazi-wa-tabora-matatani-kwa-kumiliki.html
0 Response to "MKAZI WA TABORA MATATANI KWA KUMILIKI KIWANDA CHA BUNDUKI."
Post a Comment