Tume ya Uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo majimbo 3 na kata 6

Tume ya Uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo majimbo 3 na kata 6 - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Tume ya Uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo majimbo 3 na kata 6, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Tume ya Uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo majimbo 3 na kata 6
kiungo : Tume ya Uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo majimbo 3 na kata 6

soma pia


Tume ya Uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo majimbo 3 na kata 6



Hussein Makame-NEC

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza ratiba ya Uchaguzi Mdogo katika majimbo ya Singida Kaskazini, Longido na Songea Mjini na kata sita za Tanzania Bara ambao utafanyika tarehe 13 Januari mwaka 2018.

Akitoa taarifa kwa umma jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa NEC, Mhe. Jaji Mkuu (Mst. Zanzibar) Hamid Mahmoud Hamid, alisema Tume imetangaza uchaguzi huo kufuatia kupokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu kuwepo nafasi wazi ya jimbo la Singida Kaskazini kufuatia kuvuliwa uanachama wa CCM mbunge wa jimbo hilo Lazaro Nyalandu na hivyo kupoteza sifa ya kuwa mbunge.

Kwa upande wa Jimbo la Songea Mjini, Jaji Mst. Hamid alisema kuwa Spika aliitaarifu Tume kuwepo nafasi wazi ya jimbo hilo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Leonidas Gama huku Tume ikipokea Hati ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ikithibitisha kuwa Jimbo la Longido kuwa wazi baada ya kufuta matokeo ya uchaguzi wa jimbo hilo.

Aliongeza kuwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, aliitaarifu Tume kuwepo nafasi wazi za madiwani katika kata sita Tanzania Bara.

Mhe. Jaji Mst. Hamid alizitaja kata zinazohusika katika uchaguzi huo kuwa ni Kimandolu (Halmashauri ya Jiji la Arusha), Kihesa (Halmashauri ya Manispaa ya Iringa), Bukumbi (Halmashauri ya Wilaya ya Uyui), Kurui (Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe), Keza (Halmashauri ya Wilaya ya Ngara) na Kwagunda (Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe).



Hivyo makala Tume ya Uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo majimbo 3 na kata 6

yaani makala yote Tume ya Uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo majimbo 3 na kata 6 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Tume ya Uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo majimbo 3 na kata 6 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/tume-ya-uchaguzi-yatangaza-uchaguzi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Tume ya Uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo majimbo 3 na kata 6"

Post a Comment