title : SHIRIKA LA AGPAHI LIKISHIRIKIANA NA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA WAENDESHA ZOEZI LA UPIMAJI WA VVU KATIKA VITUO VYA AFYA JIJINI TANGA
kiungo : SHIRIKA LA AGPAHI LIKISHIRIKIANA NA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA WAENDESHA ZOEZI LA UPIMAJI WA VVU KATIKA VITUO VYA AFYA JIJINI TANGA
SHIRIKA LA AGPAHI LIKISHIRIKIANA NA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA WAENDESHA ZOEZI LA UPIMAJI WA VVU KATIKA VITUO VYA AFYA JIJINI TANGA
Shirika la Ariel Glaser Pediatric AIDS Health Care Initiative (AGPAHI) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Tanga wameendesha zoezi la upimaji vya virusi vya Ukimwi kwa wakazi wa Jiji hilo huku zaidi ya wakazi 1900 wakijitokeza kupima na kupatiwa ushauri wa namna ya kuweza kujikinga na maambukizi ya VVU .
Upimaji huo ulifanyika kwenye vituo vya Afya Makorora, Ngamiani, Pongwe na Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo ikiwa ni kilele cha maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani inayoadhimishwa kila mwaka hapa nchini. Zoezi hili la upimaji lililenga wanafamilia wa watu wanaoishi na VVU katika jiji la Tanga. Upimaji huo ulianza siku ya Jumatano hadi Ijumaa (29 Novemba – 01 Disemba) ambayo ndiyo siku ya Ukimwi duniani.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baada ya kupima afya zao mkazi mmoja wa Donge Jijini Tanga, Zilipa Elangwe alisema zoezi hilo limekuwa ni zuri kwa sababu linasaidia watu kuweza kujua afya zao na namna ya kujikinga.
Alisema wanapokuwa wakijua afya zao inawasaidia kuweza kujiepusha na vitendo ambavyo vinaweza kupelekea kuingia kwenye maambukizi ikiwemo kujiepusha na ngono zembe.
Aidha alisema huduma hiyo ya upimaji wa VVU ambayo imetolewa na Shirika la AGPAHI likishirikiana na halmashauri ya jiji la Tanga imewasaidia kujua afya zao kutokana na baadhi ya familia kutokuwa na uwezo wa kifedha kwenda kupima mara kwa mara hivyo ni jambo nzuri.
“Kwa kweli tunalishukuru sana Shirika la AGPAHI kwa kutuletea huduma hii ya upimaji wa VVU maana imetusaidia kujua afya zetu lakini pia kuchukua tahadhari ya kuhakikisha tunaepukana na maambukizi mapya “Alisema.
Kushoto ni Muuguzi wa kituo cha Afya Ngamiani Lea Kakunya akichukua maelezo ya mkazi wa Jiji la Tanga ambaye alijitokeza kupima VVU wakati wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani.
Wakazi wa Jiji la Tanga wakiingia kwenye viwanja vya Kituo cha Afya Ngamiani kwa ajili ya kupima VVU katika zoezi ambalo liliendeshwa na Shirika la AGPAHI katika vituo vya Afya vya Makorora,Ngamiani ,Pongwe na Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo ambapo zaidi ya wananchi 1900 walijtokeza kupima.
Kushoto ni Ochieng Makaranga ambaye ni Mratibu wa Huduma na Tiba kwa watu wenye VVU Kituo cha Afya Ngamiani Jijini Tanga akichukua maelezo ya mkazi wa Jiji hilo wakati wa zoezi la Upimaji wa VVU jana Desemba Mosi
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Tanga wakiwa kwenye kituo cha Afya Makorora wakisubiri huduma ya kupima VVU.
Hivyo makala SHIRIKA LA AGPAHI LIKISHIRIKIANA NA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA WAENDESHA ZOEZI LA UPIMAJI WA VVU KATIKA VITUO VYA AFYA JIJINI TANGA
yaani makala yote SHIRIKA LA AGPAHI LIKISHIRIKIANA NA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA WAENDESHA ZOEZI LA UPIMAJI WA VVU KATIKA VITUO VYA AFYA JIJINI TANGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SHIRIKA LA AGPAHI LIKISHIRIKIANA NA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA WAENDESHA ZOEZI LA UPIMAJI WA VVU KATIKA VITUO VYA AFYA JIJINI TANGA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/shirika-la-agpahi-likishirikiana-na.html
0 Response to "SHIRIKA LA AGPAHI LIKISHIRIKIANA NA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA WAENDESHA ZOEZI LA UPIMAJI WA VVU KATIKA VITUO VYA AFYA JIJINI TANGA"
Post a Comment